22 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
22 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2024
22 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2024, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Jumamosi July 13,2024 Limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita uliofanyika May mwaka huu 2024 ambapo pamoja na mambo mengine limefuta matokeo yote ya Watahiniwa 22 (17 wa Shule na 5 wa Kujitegemea) ambao walibainika kufanya udanganyifu katika Mtihani.
Amesema kuwa watahiniwa hao walibainika kuingia na simu kwenye vyumba vya mtihani, kukutwa na notisi na wengine kusaidiana kufanya mitihani.
Kwa mujibu wa Dk Mohamed, tathmini ya udanganyifu inaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na imani yao itafika wakati itakwisha.
Katibu Mtendaji huyo wa NECTA, amesema ufaulu wa jumla kwa Masomo yote ni asilimia 96.84 huku somo lililoonekana kuendelea kuwa mwiba kwa watahiniwa ni Basic Alliance Mathematics (BAM) ambalo ufaulu wake ni asilimia 78.
Katika matokeo hayo, Baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 326, kati ya hao 304 wa mtihani wa kidato cha sita, 12 wa ualimu na tisa mtihani wa stashahada ya ualimu wa sekondari wamezuiliwa kutokana na matatizo ya kiafya.
Hata hivyo, Dk Mohamed amesema kuwa vitendo vya udanganyifu katika mitihani hiyo vimeendelea kudhibitiwa na kupungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
“Matukio ya udanganyifu wa kimkakati kwa sasa hayapo yameendelea kudhibitiwa na ndio maana unaona leo hata hatujatangaza shule yoyote ambayo imejihusisha na udanganyifu badala yake ni kutokana na wanafunzi wenyewe,” amesema Dk Mohamed.