610 Waitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Biharamulo July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
610 Waitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Biharamulo July 2024
610 Waitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Biharamulo July 2024,Kutakuwa na zoezi la Uandikishaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura litalotarajia kuanza tarehe 05/08/2024 hadi tarehe 12/08/2024 kwa muda wa siku saba tu.
Hivyo, Afisa Mwandikishaji Jimbo la Biharamulo Magharibi anapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi ya kazi ya muda ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki wote waliokidhi sifa na kuitwa kwenye usaili, kuwa usaili huo utafanyika tarehe 22/07/2024 siku ya Juma tatu saa 3:00 asubuhi katika Shule ya Msingi Biharamulo iliyopo Kata ya Biharamulo Mjini.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye Usaili wanapaswa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo:-
- Kuja na kitambulisho kinachokutambulisha kama vile NIDA au Kadi ya Mpiga kura.
- Kuja na vyeti vya Elimu kidato cha nne na kuendelea
- Kila msailiwa atajigharimia kwa chakula, usafiri na malazi.
- Waombaji kazi ambao majina yao hayataonekana katika Tangazo hili wasisite kuomba tenda pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia Masharti ya Tangazo husika
Orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili imeambatishwa kwenye PDF hapa chini;
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA JIMBO LA BIHARAMULO MAGHARIBI
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: 610 Waitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Biharamulo July 2024