KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB
KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB
KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB,Orodha ya Kozi Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo 2024/2025, Kozi Zenye Kipaumbele Kwa Wanafunzi Wanaotarajia kuomba Mkopo wa Masomo 2024/2025,Kozi Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB 2024/25.
Programu/Kozi zote za shahada zilizoidhinishwa zitawekwa katika Makundi Matatu yanayoakisi Vipaumbele vya Kitaifa kama ilivyofafanuliwa katika Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza Ujuzi (NSDS) kama ilivyoelezwa hapa chini.
KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB katika kundi la kwanza.
- Ualimu wa Sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia), Ualimu wa Hisabati na TEHAMA;
- Sayansi za Afya (Udaktari, Upasuaji Meno, Madawa ya Mifugo, Ufamasia, Uuguzi, Ukunga, Shahada ya Sayansi katika Prosthetikia na Mifupa, Shahada ya Sayansi katika Mazoezi ya Viungo, Shahada ya Sayansi ya Afya na Maabara, Shahada ya Sayansi ya Maabara na Matibabu na Shahada ya Sayansi ya Teknolojia ya Mionzi;
- Programu za Uhandisi (Ujenzi, Mitambo, Umeme, Uchimbaji Madini, Utengenezaji Nguo, Kemikali na Usindikaji, Kilimo, Chakula na Usindikaji, Magari, Viwanda, Usafiri Majini, Teknolojia ya Uhandisi wa Baharini, Elektronikia na Mawasiliano, Usindikaji na Huduma baada ya Mavuno, Maji na Umwagiliaji, na Uhandisi wa Ndege;
- Jiolojia ya Petroli, Kemia ya Petroli; mafuta na gesi
- Kompyuta, Programu za Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mitandao,
- Takwimu Bima (Actuarial and Data sciences) Kilimo, Misitu, Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji.
2: KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB Kundi la Pili
- Programu za Msingi za Sayansi (Shahada ya Sayansi kwa ujumla katika Wanyama, Mimea, Kemia, Fizikia, Baiolojia, Baiolojia ya Viumbe Vidogo, Baiolojia ya Mifugo na Bioteknolojia, Uvuvi na Mifugo, Sayansi ya Mazingira na Uhifadhi, Matibabu, Hisabati na Takwimu, Sayansi ya Mazingira na Usimamizi, Afya na Mazingira, Baioteknolojia na Maabara, Wanyamapori na Uhifadhi, na Kompyuta); TEHAMA, Vipimo na Mizani, Mazingira na Maendeleo ya Miji.
- Programu ya Sayansi ya Ardhi (Ubunifu Majengo, Ubunifu Mandhari nje ya Majengo, Usanifu ndani ya Majengo, Uchumi Ujenzi, Mipango Miji na Vijiji, Usimamizi na Uthaminishi Ardhi, Jiospasho, Teknolojia katika Usanifu).
3:KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB Kundi la Tatu
- Programu katika kundi hili ni pamoja na Masomo ya Biashara na Uongozi, Sayansi za Jamii, Sanaa, Sheria, Lugha, Fasihi na Masomo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano.
- Programu nyingine zote ambazo hazijaorodheshwa katika kundi lolote kati ya hayo matatu, zitaangukia katika kundi la tatu.
Mambo ya Kuzingatia Wakati wa kuomba Mkopo HESLB Bodi ya Mikopo
Waombaji Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2024/2025 wanafahamishwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo huu wa mwaka wa masomo 2024/2024;
- Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne iwe sawa kwenye maombi ya mkopo na udahili wa chuo;
- Waombaji ambao wamefanya mitihani ya kidato cha nne zaidi ya mara moja wahakikishe wanaorodhesha namba zote katika maombi yao;
- Kuhakikisha kuwa nyaraka zote za maombi ya mkopo unazowasilisha ziwe zimehakikiwa na mamlaka husika;
- Kuhakikisha kwamba vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo vinathibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au wakala Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali huo;
- Kuhakikisha vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo kwa Wanafunzi waliozaliwa nje ya nchi au wazazi waliofariki nje ya nchi vithibitishwe na ofisi za ubalozi husika zilizopo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Waombaji wajaze fomu zao kwa usahihi kabla ya kuziwasilisha;
- Maombi ya mikopo yanapaswa kuwa na taarifa sahihi na za kweli;
- Waombaji wote wanatakiwa kutunza nakala ya fomu ya maombi ya mkopo waliyowasilisha Bodi ya Mikopo kwa matumizi mengine (kama itahitajika);
Soma HESLB Muongozo wa Maombi ya Mikopo 2024/2025
Miongozo ya Utoaji Mkopo na Muda wa dirisha la maombi kuwa wazi
Miongozo mitano ya utoaji mikopo iliyozinduliwa Mei 27, 2024 na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (Mb), kuwa ni pamoja na;
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Awali (Bachelor) kwa 2024 -2025,
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada (Diploma) kwa 2024 – 2025,
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Stashahada ya Umahiri katika Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo kwa 2024 – 2025 (Post Graduate Diploma in Legal Practice),
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Shahada za Umahiri na Uzamivu, na
- Mwongozo wa Utoaji Ruzuku za Samia kwa mwaka 2024 – 2025
Aidha HESLB ilimejipanga kutoa huduma kwa waombaji mikopo kwa kuwa na dawati maalum la kusaidia wateja wanaokwama wakati wa kujaza maombi yao au kuhitaji ufafanuzi zaidi kwa kupiga simu kwenye namba 0736 665 533 au kutuma ujumbe wa “WhatsApp’’ kwenda namba 0739 665 533.
Katika mwaka wa fedha wa 2024/2025, serikali imetenga TZS 787 bilioni kwaajili ya mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 250,000.
Idadi hii ya wanafunzi imeongezeka kutoka wanafunzi 224,056 mwaka 2023/2024.
Hivyo, kwa mwaka ujao wa masomo kutakuwa na ongezeko la jumla ya wanafunzi 25,944.
Tags: KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB, Kozi Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB 2024/25., Kozi Zenye Kipaumbele Kwa Wanafunzi Wanaotarajia kuomba Mkopo wa Masomo 2024/2025, Orodha ya Kozi Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo 2024/2025