RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


SIMBA Mabingwa Kombe la Muungano 2024

Filed in Michezo by on 27/04/2024

SIMBA Mabingwa Kombe la Muungano 2024

SIMBA Mabingwa Kombe la Muungano 2024,Simba Mabingwa wapya Kombe la Muungano 2024, Simba Mabingwa Ligi ya Muungano 2024, Simba yatwaa Kombe la Muungano 2024, Simba Mabingwa Muungano Cup 2024.

SIMBA Mabingwa Kombe la Muungano 2024

SIMBA Mabingwa Kombe la Muungano 2024,Simba Mabingwa wapya Kombe la Muungano 2024, Simba Mabingwa Ligi ya Muungano 2024, Simba yatwaa Kombe la Muungano 2024, Simba Mabingwa Muungano Cup 2024.

Klabu ya Simba imefanikiwa kubeba Ubingwa wa Kombe la Muungano mwaka 2024 baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam fc katika mchezo wa Fainali uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar.

Bao la ushindi lililoipa Simba Ubingwa huo lilipatikana kipindi cha pili kupitia kwa kiungo Babacar Sarr aliyefunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Saido Ntibazonkiza.

Hii inakuwa mara ya sita kwa Simba kuchukua Kombe hilo, sawa na Yanga ambao waligoma kushiriki michuano hii mwaka huu wa 2024.

Ubingwa huo unaifanya Simba iondoke na Tsh50 milioni ambazo ni zawadi ya mshindi wa michuano hiyo.

Kombe la Muungano lilianzishwa mwaka 1982 na kufa mwaka 2003 kabla ya kurejea tena mwaka huu 2024.

Simba ilifika Fainali hiyo baada ya Kupata Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, huku Azam FC ikitinga Fainali baada ya Ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya KMKM.

Aidha Klabu ya Azam FC ambayo imeshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza imeondoka na Tsh30 milioni kama Mshindi wa pili.

Katika hatua nyingine, Kiungo Mshambuliaji Saido Ntibazonkiza amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ambapo ameondoka na kitita cha Tsh 300,000.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Saido alisema ushindi huo utarejesha ari ya timu ambapo amesema wataendelea kupambana ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zilizosalia kuhitimisha msimu huu wa 2023/2024.

Aidha Saido amewataka Mashabiki wa Simba kuendelea kuiunga mkono timu yao katika nyakati zote.

Tuzo ya kipa bora wa Mashindano imekwenda kwa Ayoub Lakred wakati mchezaji bora wa michuano hiyo ni Fabrice Ngoma.

Mfungaji Bora wa Mashindano hayo Abdul Suleiman Sopu wa Azam FC, ambaye alifunga mabao 2 dhidi ya KMKM sawa na  Abraham Alli wa KMKM ambaye timu yake imeshatolewa.

MABINGWA WA LIGI YA MUUNGANO: 1982-2024.

1.Simba SC mara 6 (1993, 1994, 1995, 2001, 2002 na 2024).

2.Yanga SC mara 6 (1983, 1987, 1991, 1996, 1997 na 2000).

3.Majimaji FC mara 3 (1985,1986 na 1998).

4.Malindi FC mara 2 (1989 na 1992).

5.Pan African mara 1 (1982).

6.KMKM mara 1 (1984).

7.Tanzania Prisons mara 1 (1999).

8.African Sports mara  1 (1988).

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , ,

Comments are closed.