ABDULRAZACK Mohamed Hamza ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
ABDULRAZACK Mohamed Hamza ni Mnyama
ABDULRAZACK Mohamed Hamza ni Mnyama, Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati, Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka miwili.
Abdulrazack ni mchezaji kijana wa Kitanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini kwa ubora mkubwa akiwa kwenye kikosi cha kwanza.
Abdulrazack mwenye umri wa miaka 21 bado ana nguvu na muda mrefu wa kucheza soka hivo Simba inaamini atakuwa msaada mkubwa ndani ya timu hiyo.
Ukiacha ubora alionao na umri wake Abdulrazack ni mchezaji ambaye anaijua vizuri Ligi ya Tanzania kwakuwa amecheza kwa ubora katika timu za Mbeya City, KMC FC na Namungo FC.
Abdulrazack ametua Simba kuongeza uimara katika idara ya ulinzi wa kati ambapo anaungana na Che Fondoh Malone na Lameck Lawi.
Abdulrazack anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi baada ya Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.