ABOUTWALIB Mshery Asaini Mkataba Mpya
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
ABOUTWALIB Mshery Asaini Mkataba Mpya
ABOUTWALIB Mshery Asaini Mkataba Mpya, Golikipa Aboutwalib Mshery ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia Young Africans SC.
Mshery aliyejiunga na Young Africans kipindi cha usajili wa dirisha dogo msimu wa 2021-2022, yupo ndani ya mipango ya timu katika kuendelea kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao wa 2024/2025.
Mshery amekuwa mbadala sahihi wa Kipa nambari moja wa Klabu hiyo, Djigui Diarra anapokosekana ambaye pia naye ameongezewa Mkataba wa miaka miwili pindi anapokosekana.
Msimu uliopita kipindi cha michuano ya AFCON wakati Diarra alipokuwa na majukumu ya kuitumikia Timu ya Taifa ya Mali, Mshery alisimama imara langoni na kuendelea kuifanya timu kubaki kwenye mstari wa kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.
Katika kipindi cha misimu miwili na nusu aliyokuwa ndani ya Young Africans SC, Mshery ameshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC mara tatu, Kombe la FA mara tatu na moja Ngao ya Jamii.