AHMED Ally Awaita Mashabiki Simba Day August 03-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
AHMED Ally Awaita Mashabiki Simba Day August 03-2024
AHMED Ally Awaita Mashabiki Simba Day August 03-2024,Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewaomba Wanasimba kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 3 katika Tamasha la kihistoria la Simba Day.
Ahmed amesema kuwa Simba Day ya mwaka huu itakuwa tofauti kuanzia mpangilio, burudani mpaka aina ya kikosi walichonacho.
Ahmed ameyasema hayo katika Tawi la Full Support Mwananyamala Kichangani alipokuwa akiendelea na hamasa kuelekea Simba Day.
“Msimu huu Simba Day ni ya tofauti. Mwanasimba mwenzangu Simba Day hii sio ya kuangalia kwenye TV.”
“Jean Charles Ahoua, Joshua Mutale na Debora Fernandes sio wa kuwaangalia kwenye TV, hawa inabidi tukawatazame uwanjani.”amesema Ahmed.
Akizungumzia kuhusu tiketi Ahmed amesema “ninachowashauri ni kununua tiketi mapema ili msikose burudani, tuna kikosi imara na msimu huu tutakuwa na furaha.”