AISHA Masaka Atua Brighton ya Uingereza
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
AISHA Masaka Atua Brighton ya Uingereza
AISHA Masaka Atua Brighton ya Uingereza,Klabu ya BK Hacken ya Sweden imemuuza Mshambuliaji, Aisha Masaka raia wa Tanzania kwenda klabu ya Brighton inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Uingereza.
Hacken imetoa taarifa kuwa imemuuza mchezaji huyo kujiunga na Brighton inayoshiriki Ligi ya Kuu ya Wanawake nchini Uingereza ambayo imemaliza nafasi ya tisa kwenye Msimamo wa Ligi hiyo ya Wanawake Msimu uliopita wa 2022/2023.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa wanawake Tanzania, Twiga Stars, alijiunga na Hacken msimu 2022 akitokea Yanga Princess.
Masaka aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya Kwa upande wa soka la wanawake, akiwa amedumu kwa misimu miwili huku akifanikiwa kufunga mabao manne msimu uliopita wa 2023/2024.
Mtanzania huyo msimu ujao wa 2024/2025 atacheza Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 12 ikiwemo, Manchester United, Manchester City, Arsenal na Chelsea.
Nyota ya mshambuliaji huyo ilianza kuonekana akiwa na Alliance Girls ya Mkoani Mwanza ambako alicheza kwa misimu mitatu kuanzia 2018/2021.
Msimu uliofuata Yanga ikamsajili akitokea Alliance ambako alifanya vizuri sana, ambapo msimu wa 2021/2022 aliibuka Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania hivyo kushinda tuzo ya kiatu cha dhahabu akiweka kambani mabao 35, akifuatiwa Mtanzania mwenzake, Opah Clement aliyefunga mabao 34.
Msimu uliofuata Yanga ikamuuza kwenda Sweden ambako licha ya kutocheza kikosi cha kwanza aliweka rekodi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.