AISHI Manula Kurejea Azam FC
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
AISHI Manula Kurejea Azam FC
AISHI Manula Kurejea Azam FC , Aliyekuwa kipa namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula hatokuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao wa 2024/2025 baada ya kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Azam FC.
Manula ambaye amedumu kwa misimu saba ameichezea Simba kwa mafanikio makubwa tangu alipotua klabuni hapo mwezi Agosti mwaka 2017, akitokea Azam FC.
Kipa huyo ambaye msimu ulioisha haukuwa mzuri kwake kutokana na kusumbuliwa na jeraha la nyonga anatajwa kurejea Azam FC msimu ujao akiungana na kipa namba moja wa timu hiyo aliyeongezwa mkataba Mohamed Mustafa aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Al Merrikh ya kwao Sudan.
Aidha Azam imefikia hatua hiyo ya kumrejesha Manula mwenye umri wa miaka 28 baada ya kuachana na Makipa wake, Abdulai Iddrisu na Ali Ahamada baada ya kuonekana watakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha mbalimbali waliyoyapata mwaka jana.