ALI Kamwe Yanga haina Kesi FIFA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
ALI Kamwe Yanga haina Kesi FIFA
ALI Kamwe Yanga haina Kesi FIFA, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kuwa klabu hiyo haina kesi yoyote FIFA baada ya kumalizana na wachezaji waliokuwa wana madai.
Kamwe amesema tayari klabu imepokea taarifa ya uthibitisho kutoka FIFA kuhusu kukamilisha kwa madai ya wachezaji Mamadou Doumbia na Lazarus Kambole.
“Tarehe 14 Juni, yaani siku moja kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, tulifanya malipo ya madai yote tuliyokuwa tunadaiwa na wachezaji FIFA”
“Kiufupi ni kwamba hatuna kesi yoyote ya madai kutoka kwa mchezaji yeyote FIFA. Tumekamilisha malipo ya Kambole na hata FIFA wenyewe wamethibitisha”
“Tatizo lililotokea ni mchezaji mwenyewe (Kambole) hajaingia katika mfumo wa FIFA kuthibitisha kupokea malipo hayo. Hivyo FIFA wametoa siku tano kwa mchezaji huyo kuthibitisha na kifungo kitaondolewa,” alisema Kamwe
Akizungumzia mchezaji Augustine Okrah, Kamwe amesema klabu itatoa taarifa kuhusu mchezaji huyo pale wakati utakapofika
Aidha Kamwe amesema kuwa taarifa za Usajili wa Yanga zitaanza kutolewa Julai 01 pale michakato yote itakapokuwa imekamilika
“Tutaanza kutoa taarifa za usajili Julai 01, kuna wachezaji tumewasajili lakini mpaka sasa timu zao za zamani hazijawapa barua za ‘release’. Yaani wachezaji wamemaliza mikataba lakini hawataki kuwapa barua”
“Hivyo tunasubiri kukamilika kwa taratibu zote muhimu kabla ya kuanza kutangaza taarifa zao,” aliongeza Kamwe