ALLY Kamwe athibitisha Aziz Ki hajasaini Mkataba Mpya
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
ALLY Kamwe athibitisha Aziz Ki hajasaini Mkataba Mpya
ALLY Kamwe athibitisha Aziz Ki hajasaini Mkataba Mpya,Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa Mchezaji wao kutoka Burkina Faso, Stephen Aziz KI Mkataba wake na Yanga SC unamalizika mwisho wa msimu huu ila wapo kwenye Mazungumzo nae.
“Mimi siwezi kuwekeza nguvu kwenye siasa na sitaki kudanganya Wanachama wa Yanga, nawaambia uhalisia mapema wajue nini tunatakiwa tufanye”
“Aziz Ki ni Mchezaji wa Yanga ana Mkataba hadi mwisho wa msimu, mpaka sasa hivi tuko kwenye mazungumzo nae lakini Aziz KI hajasaini Mkataba mpya huo ndio ukweli sitaki kuwekeza kwenye siasa”
Hadi sasa Aziz KI amekuwa akihusishwa kuwindwa na Vilabu vya Mamelod Sundowns na Kaizer Chiefs vya Afrika Kusini pamoja na Club moja wapo ya Qatar.
“Mambo mnayoyasikia sisi hatutaki kuyaongelea Kwa sababu tunajua Hapa Tanzania hakuna Timu inayoweza kumsajili Aziz Ki
Ila tunajua watu wanaomtaka Aziz Ki wapo vizuri Financial hiyo ni kweli Sina haja ya kufanya Propaganda tofauti yangu Mimi Msemaji na wasemaji wengine Nimenyooka kama Rula
Ningekuwa mtu wa propaganda ningewaambia Aziz Ki Tayari yupo Yanga, Ukweli Hayupo Bado Jukumu letu Mimi na wewe Mwana Yanga kuhakikisha Tunajisajili Aziz Ki anabakia Yanga Hiyo ndiyo Fact hakuna Siasa Hapa Tusidanganyane Wala tusipeane moyo wakati Uhalisia tuna ukimbia” Aiongeza Ally Kamwe.