Amina Bilal ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Amina Bilal ni Mnyama
Amina Bilal ni Mnyama, Klabu ya Simba Queens imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo fundi, Amina Bilal Kutoka JKT Queens.
Amina ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa soka la Wanawake akiwa amecheza timu tofauti nchini na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars).
Usajili wa Amina kwenye kikosi Cha Simba Queens unaenda kuongeza nguvu kuanzia kwenye Michuano ya ndani hadi Kimataifa ambayo Simba Queens itashiriki.
Msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Wanawake (Tanzania Women’s Premier League 2023/2024) Amina alifanikiwa kufunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine sita (Assisti).
Kama ilivyokuwa kwenye timu ya wanaume ya Simba SC hata Simba Queens imefanya maboresho makubwa ya kikosi hicho lengo likiwa kuandaa kikosi imara msimu wa 2024/25.
Katika msimu wa 2021/22 Amina alichaguliwa mchezaji bora Ligi (MVP) na msimu wa 2022/23 akachaguliwa katika kikosi bora cha msimu..
Aidha Simba Queens imeachana na wachezaji 10 Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25.
Wachezaji Walioachwa na Simba Queens ni
Zubeda Mgunda
Zainabu Mohamed
Koku Kipanga
Wema Richard
Silvia Thomas
Diana Mnally
Danai Bhobho
Joanitah Ainembabazi
Diakiese Kaluzodi
Olaiya Barakat
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Amina Bilal ni Mnyama