AZAM FC Yasajili Mshambuliaji Kutoka Colombia
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
AZAM FC Yasajili Mshambuliaji Kutoka Colombia
AZAM FC Yasajili Mshambuliaji Kutoka Colombia,Baada ya kujihakikishia nafasi ya kucheza Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF Champions League msimu ujao wa 2024/2025, klabu ya Azam imeendelea kujiimarisha kwenye baadhi ya maeneo yenye mapungufu.
- SELECTION za Form Five na Vyuo vya Kati 2024
- JINSI ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2024/2025
Klabu hiyo leo imetangaza kukamilisha usajili wa Mshambuliaji, Jhonier Blanco raia wa Colombia kutoka Aguilas Doradas ya Rionegro, inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia.
Blanco aliyezaliwa October 18, 2000, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya, kufuatia Makubaliano baina yake na klabu ya Azam FC.
Taarifa ya Azam Fc imeeleza kuwa nyota huyo alianzia soka lake kwenye akademi ya Club Deportivo Estudiantil kabla ya kujiunga na timu ya ligi kuu ya Aguilas Doradas na kutolewa kwa mkopo kwenye klabu ya daraja la kwanza ya Fortaleza.
Akiwa na klabu hiyo aliibuka kuwa Mfungaji Bora na kuisaidia kupanda daraja.
Baada ya mkopo akarudi klabuni kwake Aguilas Doradas hadi sasa ambapo Azam FC imemnunua.