AZAM FC Yatinga Fainali CRDB Bank Federation Cup 2023/2024
AZAM FC Yatinga Fainali CRDB Bank Federation Cup 2023/2024
AZAM FC Yatinga Fainali CRDB Bank Federation Cup 2023/2024, Klabu ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Maarufu CRDB Bank Federation Cup baada ya Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mabao ya Azam FC kwenye Ushindi huo yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 41 kwa mkwaju wa penalti, bao jingine amefunga dakika ya 79 huku Feisal Salum Abdallah akifunga bao la tatu na la mwisho dakika ya 69.
Kwa Ushindi huo Azam FC itakutana na Mshindi wa Nusu Fainali ya Pili ya CRDB Bank Federation Cup Kati ya Young Africans dhidi Ihefu SC, Mchezo ambao utachezwa kesho Jumapili May 19-2024.
Tags: AZAM FC Yatinga Fainali CRDB Bank Federation Cup 2023/2024