AZIZ Andabwile ni Mwananchi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
AZIZ Andabwile ni Mwananchi
AZIZ Andabwile ni Mwananchi, Klabu ya Yanga SC imekamilisha Usajili wa kiungo Mkabaji, Aziz Andabwile kutoka Fountain Gate FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Usajili wa kiungo huyo ni sehemu ya kuimarisha kikosi Cha Yanga Kuelekea msimu ujao wa 2024-2025.
Andambwile anakuja Young Africans SC kuongeza nguvu eneo hilo ambalo linachezwa na Khalid Aucho na Jonas Mkude.
Kiungo huyo anasifika kwa kucheza soka la utulivu na kupiga pasi za uhakika kwa wenzake anapokuwa uwanjani.
Andabwile anakuwa Mchezaji wa tano Kusajiliwa na Young Africans baada ya Kipa, Khomeiny Aboubakar Khomeiny Kutoka Singida Black Stars, kiungo Clatous Chama Kutoka Simba SC.
Wengine ni Mshambuliaji Prince Dube Kutoka Azam FC, na beki wa kushoto Chadrack Boka Kutoka Eloi Lupopo ya nchini DR Congo.