RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA

FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA

PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

AZIZ Ki Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024

Filed in Michezo by on 28/05/2024 0 Comments

AZIZ Ki Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024

AZIZ Ki Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024, Wafungaji Bora NBC Premier League 2023/2024, Top Score NBC Premier League, Tanzania Top Scorer, Tanzania Premier league 2023/24,Top Scorers NBC Premier League 2023/2024, Stephen Aziz Ki Mfungaji Bora NBC Premier League 2023/2024.

Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Young Africans, Stephen Aziz Ki ndiye Mfungaji Bora kwenye NBC Premier League msimu huu wa 2023/24 akifunga jumla ya magoli 21.

AZIZ Ki Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024, Wafungaji Bora NBC Premier League 2023/2024, Top Score NBC Premier League, Tanzania Top Scorer, Tanzania Premier league 2023/24,Top Scorers NBC Premier League 2023/2024, Stephen Aziz Ki Mfungaji Bora NBC Premier League 2023/2024.

AZIZ Ki Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024

Pamoja na Ufungaji Bora, Aziz Ki mzaliwa wa Abidjan, Ivory Coast raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 28 pia ametoa pasi za mabao 8 na kufanya ahusike kwenye magoli 29 kati ya 71 ya Young Africans msimu huu wa 2023/2024.

Nyuma yake yupo Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum aliyemaliza na magoli 19 huku nafasi ya 3 ikichukukuliwa na Wazir Junior wa KMC FC akimaliza na mabao 12.

Max Nzengeli wa Young Africans na Saido Ntibanzonkiza wa Simba SC wameshika nafasi ya 4 kwenye orodha hiyo ya Wafungaji Bora msimu huu w 2023/2024 Kwa kumaliza na mabao 11 kila mmoja.

Nafasi ya 5 imechukukuliwa na Kiungo wa Azam FC, Kipre Junior aliyemaliza na magoli 10.

Wakati Aziz na Feisal wakiwa sawa kwa mabao, Mashabiki wengi wa Soka nchini walikuwa wakijiuliza itakuwaje kama wakimaliza msimu hivyo hivyo, lakini tayari kanuni ilikuwa imeondoa utata juu ya hilo.

AZIZ Ki Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024

Kanuni ya (13:1) kuhusu Mshindi wa Tuzo ya Mfungaji Bora inaeleza, kuwa ikiwa wachezaji zaidi ya mmoja wamefungana idadi ya mabao njia ya kwanza itakayotumika wataangalia mabao yaliyofungwa kwa njia ya kawaida yatapewa alama mbili (2).

Mabao yatakayofungwa kwa njia ya penalti yatapewa alama moja (1) na ikiwa watalingana pia itatumika kanuni ya (13:2) inayoelezea Mchezaji aliyecheza dakika chache atakuwa mshindi na ikitokea wakalingana pia itaangaliwa kanuni ya (13:3).

Kanuni hiyo ya (13:3) inaeleza, kuwa kama vigezo vyote vilivyowekwa vinafanana pia basi, Mchezaji aliyefunga mabao mengi ugenini atakuwa mshindi.

Kutokana na hilo, wakati Wachezaji hao walipokuwa na idadi sawa ya mabao Aziz Ki alikuwa amefunga penalti tatu huku Fei Toto akiwa amefunga moja.

Aziz Ki amefanikiwa kuishinda vita hiyo baada ya kumzidi Feisal mabao mawili akifunga Matatu (Hattrick) dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga ikiibuka na  ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mabao hayo 21 yanamfanya Aziz Ki kuingia kwenye orodha ya Wafungaji Bora wa Ligi Kuu waliofunga mabao 20 na kuendelea kama ilivyokuwa kwa Emmanuel Okwi (Simba – 20), Meddie Kagere (Simba – 23 na 22) na Abdallah Juma (Mtibwa SUgar – 25).

Mbabe wao ni Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika Ligi Kuu Tanzania akifunga mabao 26, rekodi hiyo aliiweka mwaka 1997 akiwa anaitumikia Yanga.

Aidha Aziz Ki ameifikia rekodi ya Amissi Tambwe aliyefunga mabao mengi (21) katika Ligi ndani ya Yanga akifanya hivyo msimu wa 2015-2016.

Tags: , , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *