RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

BAKWATA Yatangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid el Adhhaa 2024

Filed in Habari by on 09/06/2024 0 Comments

BAKWATA Yatangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid el Adhhaa 2024

BAKWATA Yatangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid el Adh’haa 2024

BAKWATA Yatangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid el Adh’haa 2024

BAKWATA Yatangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid el Adhhaa 2024, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema kuwa Sikukuu ya Eid el Adh’haa itakuwa Jumatatu ya Juni 17 na sala yake itaswaliwa katika msikiti wa Mohamed VI uliopo Makao Makuu ya Baraza hilo Kinondoni.

Hayo ni kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 8, 2024 na Katibu Mkuu wa BAKWATA Taifa, Alhaji Nuhu Mruma.

Alhaji Mruma amesema kuwa sala ya Eid itaanza saa moja asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika pia katika msikiti huo.

“Kwa niaba ya BAKWATA, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir anawatakia maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” amesema Alhaj Mruma katika taarifa hiyo.

Eid El Adh’haa ni Sikukuu inayoadhimishwa baada ya waumini wa Kiislamu kukamilisha ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za Dini hiyo.

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *