BECHI Jipya la Ufundi la Simba SC 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
BECHI Jipya la Ufundi la Simba SC 2024/2025
BECHI Jipya la Ufundi la Simba SC 2024/2025,Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco, Fadlu Davids mkataba wa miaka miwili.
Kocha raia wa Afrika Kusini ambaye ndiye mrithi Abdelhak Benchikha amekuja pamoja na wasaidizi wake wote.
Fadlu amekuwa akifanya kazi pamoja na wasaidizi wake hao kwa takribani miaka minne jambo ambalo uongo Simba umebariki.
Makocha hao wasaidizi wa Fadlu Davids ni kama ifuatavyo:
- Kocha Msaidizi – Darian Wilken raia wa Afrika Kusini
- Kocha wa Makipa – Wayne Sandilands raia wa Afrika Kusini
- Kocha wa viungo – Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini
- Mchambuzi wa mechi – Mueez Kajee raia wa Afrika Kusini pamoja na;
- Fadluraghman “Fadlu” Davids ambaye ndiye Kocha Mkuu.