RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


CCM yateua 10 kugombea nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

Filed in Habari by on 02/09/2024 0 Comments
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

CCM yateua 10 kugombea nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

CCM yateua 10 kugombea nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana tarehe 01 Septemba 2024 katika kikao chake maalum, imefanya uteuzi wa majina ya wana-CCM 10 kugombea nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kati ya wanachama 47 walijitokeza kuwania uteuzi huo.

Wanachama walioteuliwa na Kamati Kuu ni hawa wafuatao:

  1. Ndugu Gladness Ladislaus SALEMA
  2. Ndugu Maria Alphonce SEBASTIAN
  3. Ndugu Queenelizabeth William MAKUNE
  4. Ndugu Ester Anania CHAULA
  5. Prof. Neema Penance KUMBURU
  6. Ndugu Lucia Sebastian PANDE
  7. Ndugu Fatuma Abdallah KANGE
  8. Ndugu Hawa Suleiman MKWELA
  9. Ndugu Fatma Suleiman MSOFE
  10. Ndugu Theresia Rosemary DOMINIC

Wagombea walioteuliwa, watapigiwa kura Leo Jumatatu, tarehe 2 Septemba 2024 na kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, saa 8 mchana, jijini Dodoma.

Kisha tarehe 5 Septemba 2024, kutakuwa na uchaguzi wa kumpata mbunge mmoja kwa kuchaguliwa na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Kamati Kuu imewaondoa viongozi watatu kwenye nafasi zao kwa kukiuka maadili ya uongozi.

Waliondolewa ni:

  1. Palina Ninje, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Jumuiya ya CCM, Mkoa wa Lindi.
  2. Abdul Rashid Zahoro, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
  3. Munira George Nkango, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Singida.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *