CHADRAK Boka Aumia Nyonga
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
CHADRAK Boka Aumia Nyonga
CHADRAK Boka Aumia Nyonga,Mlinzi wa kushoto wa Klabu ya Yanga, Chadrak Boka jana alishindwa kumaliza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Ausburg baada ya kupata majeraha ya nyonga.
Boka aliingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nickson Kibabage hata hivyo Kocha Miguel Gamondi alilazimika kufanya mabadiliko ya lazima kwa kumuingiza Shekhan Khamis baada ya Boka kushindwa kuendelea na mchezo.
Meneja wa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kuwa Boka alipata majeraha ya misuli ya nyonga na madaktari wanatarajiwa kumfanyia vipimo zaidi kubaini ukubwa wa jeraha hilo.
Boka ni mchezaji mpya kwenye kikosi Cha Yanga akisajiliwa kwenye dirisha hili la usajili kutokea FC Lupopo ya kwao DR Congo.