CHAMA Awaaga Simba SC
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
CHAMA Awaaga Simba SC
CHAMA Awaaga Simba SC, Kiungo Mshambuliaji, Clatous Chama ametoa ya moyoni kwa familia ya Simba Sc kupitia waraka wake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Kupitia Mitandao hiyo Chama ameishukuru Familia ya Simba ambayo amekaa nayo kwa miaka Sita kwa kuandika kuwa;
“Wapendwa familia ya Simba, Miaka sita iliyopita, nilikuja kwenu kama mgeni. Mlinipa kusudi na changamoto ya kuwa toleo bora zaidi ya nilivyokuwa.” ameandika Chama.
“Tuliteka ardhi hii pamoja, tukapanua eneo letu hadi sehemu nyingine za Afrika, na kilichobaki ni historia.”
“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na kusudi, hatima zetu zilizounganishwa huchukua uelekeo tofauti. Sina chochote ila heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na msaada mlionipa miaka yote hii, na HAKUNA MTU anayeweza kubadilisha historia tuliyotengeneza pamoja.”
“Wanasema shoo haijaisha mpaka mwanadada huyo mnene aimbe, na ninaamini huu wimbo unafaa muda kwenu. Nawatakia kila la kheri, na tutaendelea kuonana. Nguvu Moja.”
Aidha Mwamba huyo wa Lusaka amebadili wasifu (profile) kwenye mitandao ya kijamii kutoka kuwa mchezaji wa Simba Sc na kuwa mchezaji wa Yanga Sc.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: CHAMA Awaaga Simba SC