CHEICKNA Diakite Atambulishwa Azam FC
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
CHEICKNA Diakite Atambulishwa Azam FC
CHEICKNA Diakite Atambulishwa Azam FC,Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo Mshambuliaji, Cheickna Diakite kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Real Bamako ya kwao, Mali.
Diakite mwenye umri wa miaka 19 anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa Azam FC kuelekea msimu ujao wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien.
Wengine ni, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao Colombia na Mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao Colombia pia.
Wengine ni wazawa wawili, kiungo Nassor Saadun Hamoud kutoka Geita Gold na mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma.
Aidha, Azam FC pia imemnunua moja kwa moja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa wa Kimataifa was Sudan, Mohamed Mustafa kutoka El Merreikh ya Sudan.
Hatua hiyo inafuatia kazi nzuri ya kipa huyo kufuatia kusajiliwa kwa mkopo mwezi Januari akiisaidia Azam FC kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).