COASTAL Yaendeleza Mgomo kwa Lameck Lawi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
COASTAL Yaendeleza Mgomo kwa Lameck Lawi
COASTAL Yaendeleza Mgomo kwa Lameck Lawi,Mvutano kati ya Klabu za Simba na Coastal Union juu ya usajili wa beki, Lameck Lawi huenda ukamalizwa na mamlaka za juu za Usimamizi wa soka baada ya timu hizo kutofikia Makubaliano.
Aidha imeripotiwa kuwa Lawi ameripoti katika mazoezi ya kikosi cha Coastal Union kinachojiandaa kushiriki michuano ya Kagame Cup na wakati huohuo akitakiwa kuripoti Dar Es Salaam kwaajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za klabu ya Simba kabla ya kusafiri kwenda Misri kwaajili ya pre-season
Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union, Steven Mguto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, amesema kuwa klabu yake imeshamalizana na Simba kuhusu mchezaji huyo na atabaki Coastal Union FC.
“Suala la Lawi tumeshalifunga kwa sababu tangu mwanzo tulieleza Simba hawakutimiza masharti hivyo pesa yao yote ilirudishwa”
“Lawi mchezaji wetu na yuko katika kikosi kwa ajili ya maandalizi ya Kagame Cup,” alisema Mguto
Kwa Upande wa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba, Crescentius Magori yeye amesema kuwa kama hawatafikia mwafaka hapa ndani basi suala hilo huenda likaenda kuamuliwa na FIFA (CAS)
Klabu ya Simba ilimsajili Lameck Elius Lawi June 20-2024, kwa mkataba wa miaka mitatu kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Lawi mwenye umri wa miaka 18 na umbile refu alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kutambulishwa katika kikosi hicho kuelekea msimu mpya wa Ligi wa 2024/2025.