DROO ya Awali ya CAF 2024/2025 Kufanyika Leo July 11-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
DROO ya Awali ya CAF 2024/2025 Kufanyika Leo July 11-2024
DROO ya Awali ya CAF 2024/2025 Kufanyika Leo July 11-2024,CAF to conduct Preliminary Draw of 2024/25 CAF Interclub season on Thursday.
Droo ya hatua ya awali na raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) na Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) 2024/2025 inatarajiwa kufanyika Leo Alhamisi ya Julai 11, 2024 Mjini Cairo nchini Misri.
Kwa mujibu wa Kalenda ya Michuano hiyo, mechi za hatua ya awali mtoano zitaanza kuchezwa August 16 hadi 18 na Marudiano itakuwa ni August 23 hadi 25.
Mechi za raundi ya kwanza zitapigwa September wakati hatua ya Makundi itaanza October 2024.
Vilabu vya Yanga SC, Azam FC, Coastal Union na Simba SC zitaweza kuwafahanu wapinzani wao watakaokutana nao kwenye Mashindano hayo ya Pili kwa ukubwa Barani Afrika.
Yanga SC na Azam FC wataiwakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa Barani Afrika (CAF Champions League), huku Simba SC na Coastal Union zikiiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup).
Kwa Michuano ya TotalEnergies CAF Champions League 2024, Jumla ya vilabu 59 Vitashiriki kutoka nchi 47 za Afrika, huku Kombe la Shirikisho la CAF pia litakuwa na vilabu 52 vinavyowakilisha nchi 41.
Katika msimu uliopita, Mabingwa watetezi Al Ahly SC waliongeza mataji yao ya TotalEnergies CAF Champions League hadi rekodi ya kuongeza mara 12, huku wapinzani wao Zamalek wakitawazwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF kwa mara ya pili.
Ni timu 5 tu ambazo hazitakuwepo kwenye hatua ya awali kwenye Ligi ya Mabingwa, CAF Champions League 2024/2025 kutokana na kuwa katika nafasi za juu kwa viwango vya ubora vya CAF ambazo ni;
- Al Ahly ya Misri.
- Esperance de Tunis ya Tunisia
- Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini.
- Petro de Luanda ya Angola na
- TP Mazembe ya DR Congo.
Timu zingine 54 zilizobaki zitaanzia raundi ya awali (Preliminary).
Kwa Upande Wa Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup 2024/2025) ni timu 12 ambazo hazitaanzia hatua ya awali nazo ni kutokana na kuwa katika nafasi za juu kwa viwango vya ubora vya CAF ambazo ni nazo ;
- Simba SC ya Tanzania.
- RS Berkane ya Morocco.
- Zamalek ya Misri.
- ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
- Enyimba ya Nigeria
- Stade Malien ya Mali.
- USM Alger ya Algeria.
- El Masry ya Misri.
- CS Sfaxien ya Tunisia.
- AS Vita Club ya DR Congo.
- Sekhukhune United ya Africa Kusini na
- FC Lupopo ya DR Congo.
Kwa taratibu na ratiba rasmi za droo ya TotalEnergies CAF Champions League BOFYA HAPA
Kwa taratibu na ratiba rasmi za droo ya Kombe la Shirikisho la TotalEnergies CAF BOFYA HAPA
Kwa taarifa zaidi tembelea www.cafonline.com
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: DROO ya Awali ya CAF 2024/2025 Kufanyika Leo July 11-2024