EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024
EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024,EWURA Bei Mpya ya Mafuta Kuanzia April 03-2024, EWURA New Fuel Price Tanzania April 2024, New Fuel Price Tanzania April 3-2024,Energy and Water Utilities Regulatory Authority, Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta ya Petroli kuanzia Jumatano tarehe 03-04-2024.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 3 Aprili 2024 saa 6:01 usiku.
Kwa mwezi Aprili 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.
JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA (SHILINGI/LITA)Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na.3.
Kwa mwezi April 2024, mabadiliko ya bei yamechangiwa na: kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa 3.94% kwa mafuta ya petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya dizeli, kupungua kwa gharama za kuagiza mafuta (premiums) kwa wastani wa 4.28% kwa mafuta ya petroli na kuongezeka kwa wastani wa 0.76% kwa mafuta ya dizeli kwa bandari ya DSM; kuongezeka kwa wastani wa 13.73% kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Bandari ya Tanga; na kuongezeka kwa wastani wa 12.71% kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Bandari ya Mtwara.
Aidha, mabadiliko hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kwa asilimia 3.19 kutokana na ongezeko la matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa.
Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3.
Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za
mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote
atakayekiuka AGIZO hili.
EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: –
- bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.
- Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
- Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko.
- EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
- Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A la tarehe 30 Oktoba 2023 na Mabadiliko ya Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za Mwaka 2024.
- Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.
- Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja.
- Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa
ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika. - Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.
- Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa
mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa. Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya
bidhaa za mafuta ya petroli.
Bei za Mafuta ya Petroli pia inapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga *152*00#
EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania Kuanzia April 03-2024 Saa 06:01 Download PDF
Bei za Mafuta ya Petroli Kwa mwaka 2024
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd April 2024 -Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd April 2024 – English
Cap Prices for Petroleum Products wef 6th March 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 6th March 2024 – English
Cap Prices for Petroleum Products wef 7th February 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 7th February 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd January 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd January 2024- English
Kuhusu EWURA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ni taasisi ya udhibiti wa huduma za nishati na maji inayojitegemea, iliyoundwa kwa Sheria ya EWURA Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 2019.
EWURA, ilianza kazi rasmi Septemba, 2006 ikiwa na wajibu wa kusimamia shughuli zote za kiuchumi na kiufundi katika sekta za Nishati(umeme, petroli na gesi asilia); na Maji (majisafi na usafi wa mazingira).
Katika kutekeleza wajibu wake, kwa uwazi na kwa manufaa ya wote, EWURA inazingatia sheria za kisekta, sera na miongozo ifuatayo:-
Sera ya Taifa ya Nishati (2015), Sera ya Taifa ya Maji (2002), Sheria ya EWURA, Sura Na. 414; Sheria ya Umeme, Sura Na. 131; Sheria ya Petroli, Sura Na. 392; Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira, Sura Na. 279; kanuni na miongozo mbalimbali.
Dira ya EWURA
Kuwa Mdhibiti wa Kiwango cha Kimataifa kwa Huduma Endelevu za Nishati na Maji
Dhamira ya EWURA
Kudhibiti huduma za nishati na maji kwa uwazi, ufanisi na tija ili kuhakikisha ubora, upatikanaji na unafuu wa huduma hizo
Kazi na Majukumu ya EWURA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya EWURA, majukumu ya Mamlaka niajukumu hayo ni:-
- Kutekeleza kazi zote zilizoanishwa kwenye sheria ya EWURA na Sheria za Kisekta;
- Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni;
- Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma;
- Kudurusu na kusimamia bei za huduma,
- Kutunga sheria ndogo na kanuni;
- Kufuatilia maendeleo ya sekta zinazodhibitiwa kwa kuzingatia upatikanaji, ubora wa huduma, gharama ya huduma, ufanisi wa uzalishaji, uwekezaji na usambazaji wa huduma;
- Kusimamia utatuzi wa malalamiko na migogoro;
- Kutoa taarifa kuhusu kazi za udhibiti;
- Kupata maoni ya mamlaka zingine za kiudhibiti; na
- Kusimamia utekelezaji wa Sura Na 414 ilyoianzisha EWURA.
Katika kutekeleza kazi zake, EWURA ina wajibu wa kukuza ustawi wa Watanzania kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kuhimiza ushindani wenye tija na ufanisi kiuchumi;
- Kulinda maslahi ya walaji;
- Kulinda mitaji ya kifedha ya watoa huduma;
- Kuhimiza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa makundi yote ikiwamo wenye vipato vya chini,makundi maalumu na vijijini;
- Kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma na kujenga uelewa kuhusu sekta zinazodhibitiwa, ikiwamo haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazodhibitiwa, namna ya kupokea na kutatua malalamiko na migogoro na kazi, wajibu na shughuli za Mamlaka;
- Kulinda na kutunza mazingira.
Soma Zaidi:-https://www.ewura.go.tz/fuel-prices/
Bei ya mafuta ya diesel leo April 2024, Bei ya mafuta ya petrol April 2024, Ewura bei mpya April 2024,bei ya petrol Dar es Salaam April 2024,Bei ya mafuta leo tanzania April 2024,Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta ya Petroli kuanzia Jumatano tarehe April 2024 saa 6:01 usiku, Jinsi ya kuangalia bei za mafuta Tanzania, Bei ya mafuta leo tanzania, Bei za mafuta April 2024.
About Nijuze Habari Blog
About Nijuze Habari Blog, About Nijuze Habari, About Nijuze Habari 24,Nijuze Habari -| Pata Habari zote za Michezo na Usajili, Magazeti, Ratiba na Matokeo na Nafasi Mpya za Ajira, Nijuze Habari 24, Nijuze Habari Ajira, Nijuze Habari Michezo, Nijuze Habari Magazeti, Nijuze Habari Matokeo, Nijuze Habari Ratiba.
Nijuze Habari ni Blog ya Kiswahili Maarufu Duniani kwa Habari za Magazeti, Habari za Michezo, Nafasi za Ajira Mpya na Tetesi za Usajili.
Nijuze Habari inakuletea Nafasi za Kazi kila siku, Makala Mbali mbali Pamoja na Kutazama Ratiba na Matokeo ya Ligi zote Duniani, Matokeo ya EPL, Matokeo ya Bundesliga, Matokeo ya Seria A, Matokeo ya La Liga, Matokeo ya League 1, Matokeo ya NBC Premier League.
Nijuze Habari inakuwezesha kutazama Matokeo ya moja kwa moja (LIVE Updates) wakati mechi zinaendelea za Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu ya NBC na kwenye michezo ya CAF pamoja na Michezo mingine itakayoshiriki
Nijuze Habari pia inakuleta Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wafungaji Bora, Makipa Bora, Wachezaji Bora, Vikosi vya Simba na Yanga, ratiba za Simba, Yanga na Azam FC, Matokeo ya Simba SC, Matokeo ya Yanga, ratiba ya Bundesliga, ratiba ya EPL, ratiba ya Seria A, ratiba ya League 1, ratiba ya La Liga.
About Nijuze Habari Blog
Nijuze Habari pia inakuletea Matokeo ya NECTA Tanzania na Zanzibar, Yanayojiri Magazetini Kila Siku, Habari Kubwa za Magazeti Pamoja Vichwa vya Habari za Magazeti.
Matokeo ya NECTA Darasa la Nne, Matokeo ya NECTA Darasa la Saba, Matokeo ya NECTA Kidato cha Kwanza, Matokeo ya NECTA Kidato cha Nne, Matokeo ya NECTA ya Form 6 na Nyuo Mbali Mbali, Pamoja Waliochaguliwa kujiunga na Kidato Cha Kwanza na Kidato Cha Tano.
Pia Nijuze Habari inakuletea taarifa zote Bodi ya Mikopo ya Elimu Juu HESLB, Nafasi za Ajira zinazotangazwa kila Siku na Taasisi Mbalimbali kama Ajiraportal na Makampuni Mbalimbali, Wanaoitwa Kazini kila siku na Wanaoitwa kwenye Usaili Taasisi Mbalimbali za Serikalini na Makampuni kila Siku, Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania March 06-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta ya Petroli kuanzia Jumatano tarehe 03-04-2024., Energy and Water Utilities Regulatory Authority, EWURA Bei Mpya ya Mafuta Kuanzia April 03-2024, EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania April 03-2024, EWURA New Fuel Price Tanzania April 2024, New Fuel Price Tanzania April 3-2024