FADLU Davids Kocha Mkuu Simba SC 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
FADLU Davids Kocha Mkuu Simba SC 2024/2025
FADLU Davids Kocha Mkuu Simba SC 2024/2025,Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco, Fadlu Davids mkataba wa miaka miwili.
Kabla ya kujiunga na Simba msimu uliopita Fadlu mwenye umri wa miaka 43 alikuwa kocha Msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Morocco, Raja Casablanca.
Fadlu ambaye enzi zake alikuwa akicheza katika nafasi ya ushambuliaji anachukua nafasi ya Abdelhak Benchikha ambaye aliondoka wakati msimu wa 2023/2024 ukiwa unaelekea ukingoni.
Mara nyingi Fadlu amekuwa muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 ambao amekuwa akiutumia katika kila timu anayofundisha.
Aidha Fadlu analijua vema soka la Afrika kutokana na kuwahi kuzifundisha timu za Maritzburg United ya Afrika Kusini kwa nyakati tofauti pamoja na Orlando Pirates.
Mbali na kufundisha Afrika pia Fadlu amewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Lokomotive Moscow ya Urusi.
Fadlu anataraji kuwasili kesho Jumamosi akiwa na benchi lake lote la Ufundi tayari kuelekea Misri kwenye kambi ya Mazoezi (Pre Season).