FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo, Jinsi ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Mkoa Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Wiliya Kilipo,JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Kata Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Kijiji Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Mtaa Kilipo.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa vitambulisho vya Taifa vimechapishwa na kusambazwa maeneo mbalimbali.
Kadhalika, orodha ya majina ya watu wote ambao vitambulisho vyao vimechapishwa imewekwa kwenye tovuti ya Mamlaka kupitia kiunganishi https://vitambulisho.nida.go.tz
Hivyo, mwananchi ambaye hujachukua kitambulisho chako, unaweza kufahamu kwa kupitia tovuti hii Ofisi ya serikali ya Mtaa/Kijiji ambapo kitambulisho chako kipo kwa ajili ya kukichukua.
Aidha, unaweza kutembelea tovuti ya Mamlaka kupitia www.nida.go.tz kisha bofya mahali palipoandikwa Kitambulisho cha Taifa ikifuatiwa na Fahamu Kitambulisho kilipo.
Baada ya hapo ukurasa unaoonyesha mikoa utafunguka, Chagua mkoa na kufuatiwa na wilaya uliyojisajili na baadae bonyeza Kata ikifuatiwa na Kijiji/Mtaa uliokuwa unaishi wakati unajisajili.
Baada ya hapo ukurasa wenye orodha ya majina na mahali Kitambulisho chako kilipo utafunguka.
Ukiona jina lako tafadhali nenda kachukue Kitambulisho chako mahali kilipo mapema kwani baada ya mwezi mmoja kupita vitarejeshwa ofisi za NIDA za wilaya.
Hivyo utalazimika kukifuata katika ofisi ya NIDA ya Wilaya uliyojisajili.
NIDA Orodha ya Majina ambao Vitambulisho vyao vipo tayari Kila Mkoa.
CHAGUA MKOA WA MAHALI ULIPO JIANDIKISHA
NIDA VITAMBULISHO KWA NGAZI YA MIKOA | |||||
---|---|---|---|---|---|
DAR ES SALAAM | TANGA | ARUSHA | KILIMANJARO | MANYARA | GEITA |
MARA | MWANZA | KAGERA | SHINYANGA | SIMIYU | DODOMA |
SINGIDA | TABORA | KIGOMA | KATAVI | IRINGA | MBEYA |
RUKWA | RUVUMA | NJOMBE | PWANI | MTWARA | LINDI |
MOROGORO | MJINI MAGHARIBI | KUSINI UNGUJA | KASKAZINI UNGUJA | KUSINI PEMBA | KASKAZINI PEMBA |
MDA-ZANZIBAR | |||||
SONGWE |
kupata namba ya kitambulisho cha nida bofya hapa, Jinsi ya kupata kitambulisho cha nida kupitia simu yako, Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA (NIN) Online Bure, Tembelea website ya NIDA kujua kama kitambulisho chako kipo tayari.
FAHAMU UMUHIMU WA KUWA NA KITAMBULISHO CHA TAIFA
Ewe Mwananchi, sasa unaweza kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN)/Kitambulisho cha Taifa (NID) kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama :-
- Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration),
- Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN),
- Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA,
- Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport),
- Kukata Leseni ya Udereva,
- Kupata Huduma ya Afya,
- Kufungua Akaunti ya Benki,
- Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi za Fedha,
- Kujiunga na Elimu Ngazi Mbalimbali,
- Kupata Mkopo wa Elimu ya Juu,
- Hati Miliki ya Kiwanja, Nyumba n.k,
- Kujidhamini na Kudhamini Wengine,
- Kitambulisho cha Taifa kutokana na kuwa na Kisilikoni (Cheap) kinaweza Kutumika kama Pochi ya Fedha ya Kielektroniki (E-Wallet) ambako unahifadhi fedha na kufanya malipo kwa kutumia Kitambulisho Chako,
- Kitambulisho kinaweza kutumika kama ATM CARD,
- Kwenye Maingio ya Malango Kielektroniki (E-Entrace),
- Daftari la Mahudhurio la Kielektroniki (Electronic Attendance),
- Mwananchi kuondokana na Adha ya Kubeba Utitiri wa Vitambulisho kwani sasa taarifa zote Muhimu za mwananchi zitapatikana katika Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu,
- Kinaweza kutumika kama hati ya Utambuzi wa Utaifa wa wananchi wanaovuka mipaka ndani ya nchi zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.
- Vitaimarisha Utendaji Kazi Serikalini kwa Kuwa na Kumbukumbu Sahihi za Watumishi na Malipo ya Stahili zao, hasa Wanapostahafu,
- Kupata Ruzuku za Pembejeo za Kilimo Kirahisi,
- Kujisajili kwenye Chama cha Ushirika (Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Makundi mengine),
- Kupata Msaada wa TASAF unaotolewa kwa Kaya Masikini,
- Kufungua Akaunti za Benki,
- Kuomba Ajira pamoja na Huduma Nyingine Nyingi.
FAHAMU AINA ZA VITAMBULISHO VYA TAIFA.
NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu, ambavyo ni kitambulisho cha raia, kitambulisho cha mgeni mkaazi, na kitambulisho cha mkimbizi mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na anayeishi nchini kihalali.
i. Kitambulisho cha Raia
Mahitaji yake:
- Cheti cha kuzaliwa
- Cheti za elimu ya msingi,
- Pasi ya kusafiria (Pasipoti)
- Cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha iv na vi)
- leseni ya udereva
- Kadi ya bima ya afya
- Kadi ya mfuko wa hifadhi ya jamii
- Kadi ya mpiga kura
- Nambari ya mlipa kodi (Tin. No)
- Kitambulisho cha mzanzibar mkazi
- Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa
ii. Kitambulisho cha Mgeni Mkazi
Mahitaji yake:
- Pasport ya nchi anakotoka
- Kibali cha kukaa nchini kuendesha shughuli mbali mbali anazofanya mwombaji
iii. Kitambulisho cha Mkimbizi
Mahitaji:
- Hari ya Mkimbizi: Hati inayosibitisha kuwa mwombaji ana hadhi ya kuwa mkimbizi nchini
Jinsi ya kupata kitambulisho cha NIDA Online, Kupata copy ya kitambulisho cha NIDA, Jinsi ya kupata kitambulisho cha taifa kwa haraka, Jinsi ya kupata kitambulisho Cha NIDA Online Download, Jinsi ya kupata namba ya NIDA kwa haraka, Namba yangu ya NIDA, Www NIDA go tz ID Number, Namba ya NIDA kwa SMS, Jinsi ya kuangalia Taarifa zangu Za NIDA, NIDA Kitambulisho, Picha ya Kitambulisho cha Taifa, Namba ya NIDA kwa sms 2024.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Kata Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Kijiji Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Mkoa Kilipo, JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Mtaa Kilipo., JINSI ya Kufahamu Kitambulisho Chako Cha NIDA Wiliya Kilipo
Mimi nilijiandikisha tangu 2017 lakini sijapata kitambulisho hadi leo. Nimejaribu kuangalia jina langu kwenye orodha yamtaa niliojiandikisha lakini halipo. Inamaana bado hakijachapishwa au ndo kimerudishwa ofisi yawilata?