FARID Mussa Asaini Mkataba Mpya Yanga
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
FARID Mussa Asaini Mkataba Mpya Yanga
FARID Mussa Asaini Mkataba Mpya Yanga, Katika Kuendelea kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao wa 2024/2025, Klabu ya Yanga imemuongezea mkatabaFarid Mussa hadi 2026.
Farid Mussa mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani, ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Young Africans SC hadi 2026.
Nyota huyo aliyejiunga na Young Africans SC mwaka 2020, ana uwezo wa kucheza winga na beki wa kushoto.
Kutokana na uwezo wake huo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani unamfanya kuwa miongoni mwa
wachezaji muhimu kikosini ambao klabu imeamua kuendelea kubaki nao
Katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa, uongozi unaendelea wa Yanga kuboresha kikosi kwa kusajili wachezaji wapya, kuwaongezea mikataba
waliopo na kuachana na wale ambao benchi la ufundi limependekeza waachwe wakatafute Changamoto nyingine nje ya Klabu hiyo.