RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


FOMATI ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2024

Filed in Makala, Habari, NACTE, TAMISEMI by on 24/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

FOMATI ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2024

FOMATI ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2024,Download fomati ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi psle 2024, Mwongozo wa usimamizi wa mitihani pdf, Uandishi wa taarifa ya usimamizi wa mitihani, Taarifa ya usimamizi wa mtihani necta.

FOMATI ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2024

FOMATI ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2024,Download fomati ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi psle 2024, Mwongozo wa usimamizi wa mitihani pdf, Uandishi wa taarifa ya usimamizi wa mitihani, Taarifa ya usimamizi wa mtihani necta.

FOMATI YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) 2024

DIBAJI
Kitabu hiki cha fomati ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kimeandaliwa
na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kuzingatia matakwa ya Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2015. Fomati hii itaanza kutumika mwaka 2024.

Katika kitabu hiki cha Fomati kuna maboresho ya idadi ya sehemu za karatasi hususani katika masomo ya 03 Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi, 04
Hisabati, 05 Sayansi na Teknolojia na 06 Uraia na Maadili ambapo kutakuwa na sehemu tatu (03) A, B na C badala ya mbili (2) za awali ambazo ni A na B.

Maboresho zaidi yaliyofanyika katika muundo wa mtihani wa masomo yote yanayotahiniwa katika ngazi hii ya elimu ambayo ni 01 Kiswahili, 02 English Language, 03 Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi, 04 Hisabati, 05 Sayansi na Teknolojia pamoja na 06 Uraia na Maadili.

Muundo wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi utakuwa na idadi ya maswali ambayo ni tofauti kutoka somo moja hadi jingine ikilinganishwa naidadi ya awali ambapo masomo yote yalikuwa na maswali 45.

Katika maboresho hayo masomo ya 01 Kiswahili na 06 Uraia na Maadili yatakuwa na maswali sita (6) kila moja. Masomo ya 04 Hisabati na 05 Sayansi na
Teknolojia yatakuwa na maswali nane (8) kila moja. Aidha, masomo ya 02
English Language na 03 Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi yatakuwa na maswali saba (7) kila moja. Katika mitihani hiyo mtahiniwa ataandika majibu yake kwenye nafasi zilizotengwa katika karatasi ya maswali.

Fomati za mtihani zimeandaliwa kwa kufuata muundo wa sehemu tano
ambazo ni Utangulizi, Malengo ya Jumla, Umahiri Mkuu, Muundo wa Mtihani
na Umahiri utakaotahiniwa kwa kila somo. Aidha, Jedwali la utahini limewekwa mwishoni mwa fomati ya kila somo na linaonesha umahiri
utakaopimwa, ngazi za nyanja ya utambuzi, idadi ya vipengele vya maswali kwa kila umahiri mahususi na asilimia ya uzito kwa kila umahiri.

Kwa ujumla, kitabu hiki cha fomati kinatoa mwongozo kwa watunzi wa
mitihani, warekebishaji wa maswali ya mtihani na walimu wa shule za msingi
katika kuandaa mitihani inayozingatia haki, uhalali na viwango.

Baraza linasisitiza umahiri wote katika masomo yote yanayofundishwa katika ngazi ya elimu ya msingi ufundishwe kwa kuzingatia mihtasari ya masomo husika.

Fomati hii ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa namna yoyote ile
isitumike kama mbadala wa mihtasari ya masomo husika.

Baraza la Mitihani linatambua na kuthamini mchango wa watu wote
walioshiriki katika kufanya maboresho ya kitabu hiki cha fomati.

KISWAHILI
UTANGULIZI
Fomati ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi somo la Kiswahili imeandaliwa kwa kuzingatia muhtasari wa somo la Kiswahili wa mwaka 2015 ulioanza kutumika 2017 (toleo la 2019). Muhtasari huo unabainisha Umahiri Mkuu na umahiri mahususi ambao mwanafunzi
anatakiwa kuupata katika ngazi ya Elimu ya Msingi Darasa la III hadi VII.

Hivyo, mtihani wa somo la Kiswahili utakaoandaliwa kwa kutumia
fomati hii, utalenga kupima umahiri alioupata mtahiniwa kuanzia Darasa la III hadi VII.

Fomati hii ni zao la maboresho yaliyofanyika kutoka fomati ya mwaka
2020 ambayo ilikuwa na maswali 45. Hivyo, mtihani wa somo la Kiswahili utakuwa na maswali sita (6) yenye jumla ya vipengele 35 ambavyo vimetoka katika umahiri mahususi wa aina sita (6) katika umahiri mkuu wa aina mbili (2).

Lengo la maboresho haya ni kumwezesha mtahiniwa kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea duniani kote na ujenzi wa msingi wa umahiri katika masomo ya sekondari na elimu ya juu.

MALENGO YA JUMLA
Mtihani wa somo la Kiswahili utapima ni kwa kiwango gani mtahiniwa
anaweza:

  • Kusikiliza, kusoma na kuandika kwa kutumia lugha ya Kiswahili;
  • Kutumia Kiswahili fasaha katika miktadha mbalimbali;
  • Kutumia Kiswahili kupata maarifa, stadi na mwelekeo wa kijamii,
    kiutamaduni, kiteknolojia na kitaaluma kutoka ndani na nje ya
    nchi;
  • Kukuza stadi za mawasiliano ili kumwezesha mwanafunzi
    kumudu maisha yake;
  • Kujenga msingi bora na imara wa kujifunza kwaajili ya elimu ya juu na kujiendeleza binafsi kwa kutumia lugha ya Kiswahili; na
  • Kuifahamu na kuitumia lugha ya Taifa.

UMAHIRI MKUU
Mtihani utapima ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:

  • Kuwasiliana katika miktadha mbalimbali; na
  • Kuonesha uelewa wa jambo alilosikiliza au kulisoma.

MUUNDO WA MTIHANI
Mtihani wa somo la Kiswahili utakuwa na karatasi moja (1) na utafanyika kwa muda wa saa 1:40 kwa watahiniwa wote isipokuwa kwa watahiniwa wenye mahitaji maalum ambapo mtihani wao
utafanyika kwa saa 1:55. Mtihani utakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali sita (6) yenye jumla ya vipengele 35.

Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote yenye jumla ya alama 50. Sehemu A itakuwa na maswali matatu (3). Swali la kwanza na la pili yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na swali la tatu litakuwa la
kuoanisha.

  • Swali la kwanza litakuwa na vipengele vitano (5) vitakavyotokana na kifungu cha maneno/hadithi itakayosomwa na Msimamizi ambapo mtahiniwa atatakiwa kusikiliza kwa makini kisha kuchagua jibu sahihi kutoka katika machaguo.
  • Swali la pili litakuwa na vipengele 10 ambapo mtahiniwa anatakiwa kuchagua jibu sahihi kutoka katika machaguo A – E. Swali la tatu litakuwa na vipengele vitano (5) vya kuoanisha.
  • Kila kipengele katika sehemu hii kitakuwa na alama moja (1) hivyo, kufanya sehemu hii kuwa na jumla ya alama 20.
  • Sehemu B itakuwa na maswali mawili (2) ambayo ni swali la nne na la tano.
  • Swali la nne litakuwa na vipengele vitano (5) ambapo mtahiniwa atatakiwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi au kupanga sentensi katika mtiririko unaoleta mantiki na kuunda kifungu cha habari.
  • Swali la tano litakuwa la majibu mafupi lenye vipengele vitano (5) kutoka katika kifungu cha habari, hadithi au shairi.
  • Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2). Hivyo, sehemu hii itakuwa na jumla ya alama 20. Sehemu C itakuwa na swali moja (1) la utungaji lenye vipengele vitano (5) vyenye jumla ya alama 10.

UMAHIRI UTAKAOTAHINIWA
Umahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa Kiswahili ni kama ifuatavyo:

  • Kuanzisha na kuendeleza mazungumzo katika miktadha
    mbalimbali;
  • Kutumia msamiati katika kuzungumza kwa kuwasilisha hoja
    kulingana na miktadha mbalimbali;
  • Kutumia maandishi katika mawasiliano kulingana na
    miktadha mbalimbali;Kusikiliza na kuonesha uelewa wa jambo alilolisikiliza;
  • Kusoma kwa ufasaha na kuonesha uelewa wa matini aliyoisoma; na

Kutumia msamiati katika kusoma na kuchanganua mawazo yaliyowasilishwa katika matini mbalimbali.

ENGLISH LANGUAGE
INTRODUCTION
This revised Primary School Leaving Examination format for English
Language subject is based on the 2015 English Language Syllabus for
teaching standards III to VII which was effectively used in 2017 (revised in 2019). That syllabus outlines the general and specific competencies that pupils ought to acquire at the primary education
level from standard III to VII. As such, the English Language examination will assess the competencies each candidate had acquired from standard III to VII.

The revised format replaces the 2020 English Language format which
had consisted of 45 questions. This format, on the other hand, will
have 7 questions with 35 assessment items for all four specific competencies derived from three general ones. These improvements aim at enabling a candidate to cope with the development of Science and Technology, which takes place in the contemporary world and
build a competency foundation for secondary and higher education.

GENERAL OBJECTIVES
The English Language examination aims to test the candidate’s ability
to:

  • Express him/herself appropriately in a given situation;
  • Use basic skills in listening, reading and writing in English;
  • Use vocabulary through listening, reading, and writing;
  • Apply correct English grammar; and.5
  • Use the English Language in acquiring higher education and for personal advancement.

GENERAL COMPETENCIES
The examination will measure the candidate’s competencies in how to:

  • Comprehend oral and written information,
  • Communicate through writing, and
  • Use vocabulary through listening, reading and writing.

EXAMINATION RUBRIC
The examination will consist of one (1) paper of 1:40 hours. The paper for the candidates with special needs will last for 1:55 hours.This paper will comprise three sections, A, B and C, and will have

seven (7) questions with 35 items. The candidates must answer all the questions, which account for 50 marks.

Section A will consist of four (4) questions. The first question will be
based on a passage/story which the invigilator will read out aloud to
the candidates. A candidate should listen attentively to the passage and respond, accordingly, to five (5) multiple choice items. The second question will consist of five (5) short answer items that require the candidates to choose the correct answer from options A – E. The third
question will require the candidates to complete five (5) sentences (i-v)
by writing down the correct words picked from the options provided.
The fourth question will contain five (5) matching items. Each item in this section will carry one (1) mark. This section will weigh 20 marks.

NECTA FOMATI MPYA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI PSLE 2024

Section B will consist of two (2) questions (Question 5 and 6), each with five (5) items. The fifth question with five items will require candidates to fill in the blank spaces. The sixth question with five (5) items will require candidates to read and understand the written
information and, accordingly, respond to five (5) short answer items. Each item will carry two (2) marks. The section will weigh a total of 20 marks.

Section C will consist of one (1) question with five items on arranging the jumbled sentences logically or writing a composition. Each item will carry two (2) marks. The section will account for 10 marks.

ASSESSMENT COMPETENCIES
The following competencies will be assessed:

  • Listening and understanding information presented orally;
  • Developing and using vocabulary appropriately through
    listening, writing and reading;
  • Communicating simple ideas through writing; and
  • Reading and comprehending written information.

MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI
UTANGULIZI
Fomati ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi katika somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi imeandaliwa kwa kuzingatia Muhtasari wa somo hilo wa mwaka 2015 ulioanza kutumika 2017
(toleo la 2019). Muhtasari huo umebainisha Umahiri Mkuu na
Umahiri Mahsusi ambao mwanafunzi anatakiwa kuupata katika ngazi ya Elimu ya Msingi Darasa la III hadi VII. Hivyo, mtihani wa somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi utakaoandaliwa kwa kutumia fomati hii, utalenga kupima umahiri alioupata mtahiniwa kuanzia Darasa la III hadi VII. Fomati hii ni zao la maboresho yaliyofanyika kutoka fomati ya mwaka 2020 ambayo ilikuwa na maswali 45 na imeboreshwa na kuwa na maswali saba (7) yenye jumla ya vipengele 35 kutoka katika umahiri mkuu wa aina zote nane

Fomati hii pia kama ile ya awali inahusisha kumpima mtahiniwa katika ngazi zote za nyanja ya utambuzi. Lengo la maboresho haya ni kumwezesha mtahiniwa kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea
duniani kote na ujenzi wa msingi wa umahiri katika masomo ya sekondari na elimu ya juu.

FOMATI ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2024

MALENGO YA JUMLA
Mtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi unalenga kupima ni kwa kiwango gani mtahiniwa anaweza:

  • Kuthamini na kulinda mazingira na rasilimali za taifa;
  • Kuthamini uhusiano wa watu na mazingira katika jamii;
  • Kutambua na kutumia fursa zilizopo katika mazingira yake;
  • Kutambua asili ya jamii za taifa letu;
  • Kujenga misingi ya kujitegemea;
  • Kuwa mbunifu; na
  • Kutambua fursa katika mazingira yake

UMAHIRI MKUU
Mtihani utapima ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:

  • Kutambua matukio yanayotokea katika mazingira
    yanayomzunguka;
  • Kutambua misingi ya uzalendo katika jamii;
  • Kutumia ramani na elimu ya anga katika maisha ya kila siku;
  • Kufuata kanuni za kiuchumi katika shughuli za uzalishaji mali;
  • Kutumia misingi ya unadhifu;
  • Kumudu mapishi mbalimbali;
  • Kusanifu kazi za sanaa; na
  • Kutumia stadi za ujasiriamali.

MUUNDO WA MTIHANI
Mtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi utakuwa na karatasi moja (1) na utafanyika kwa muda wa saa 1:30 kwa watahiniwa wote isipokuwa kwa watahiniwa wenye mahitaji maalum ambapo mtihani wao utafanyika kwa saa 1:45. Mtihani utakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali saba (7) yenye jumla ya vipengele 35. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote. Jumla ya alama zitakuwa 50.

Sehemu A itakuwa na maswali mawili (2) yenye jumla ya vipengele 20. Swali la kwanza litakuwa la kuchagua jibu sahihi
lenye vipengele 15 vinavyoundwa na machaguo matano A-E. Swali la pili litakuwa na vipengele vitano (5) vya kuoanisha ambapo mtahiniwa atatakiwa kuoanisha maswali katika orodha A na majibu katika orodha B au kuchagua neno au maneno ya jibu sahihi kutoka katika kisanduku na kuyaandika katika nafasi ya majibu atakayopewa. Kila kipengele kitakuwa na alama moja (1), hivyo jumla ya alama katika sehemu hii itakuwa 20.

Sehemu B itakuwa na maswali manne (4), swali la tatu na la nne yenye vipengele vitatu (3) kila moja na swali la tano na la sita yenye vipengele viwili (2) kila moja. Mtahiniwa atatakiwa kujibu
vipengele vyote kwa kuandika majibu mafupi. Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2) na hivyo, kufanya jumla ya alama 20.

Sehemu C itakuwa na swali moja (1) lenye vipengele vitano (5) ambapo mtahiniwa atatakiwa kutafsiri picha/ramani/mchoro na kujibu dhana mbalimbali za kijiografia. Sehemu hii itakuwa na jumla ya alama kumi (10).

UMAHIRI UTAKAOTAHINIWA
Umahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi
za Kazi ni kama ifuatavyo:

  • Kutunza mazingira ya jamii inayomzunguka, kutunza kumbukumbu za matukio ya kihistoria na kutumia elimu ya hali
    ya hewa katika shughuli za kila siku;
  • Kudumisha utamaduni wa mtanzania, kujenga uhusiano
    mwema kwa jamii inayomzunguka na kuthamini mashujaa
    wetu;
  • Kutumia ramani katika mazingira na kufahamu mfumo wa jua;
  • Kuthamini na kulinda rasimali za nchi, kutambua shughuli za
    uzalishaji mali katika jamii, kutumia stadi za ujasiliamali na
    shughuli za kila siku;
  • Kujenga tabia ya usafi wa mwili, kutunza mavazi katika kudumisha usafi na kutunza mazingira katika kudumisha makazi safi;
  • Kutambua kanuni zinazohitajika katika mapishi, kutayarisha
    vyakula aina tofauti na kutengeneza vinywaji tofauti;
  • Kumudu misingi ya uimbaji na uigizaji, kutengeneza picha
    zenye ujumbe tofauti kwa jamii, kubuni chapa mbalimbali za
    sanaa za ufundi, kufinyanga maumbo mbalimbali na kutengeneza vitu kwa kutumia makunzi mbalimbali; na
  • Kujenga utayari wa kujifunza, kutafuta masoko ya bidhaa
    ndogo ndogo, na kutumia kanuni za usimamizi wa fedha.

HISABATI
UTANGULIZI
Fomati hii ya Mtihani wa Hisabati imeandaliwa kwa kuzingatia muhtasari wa mwaka 2015 ulioanza kutumika 2017 (toleo la 2019). Maswali ya mtihani wa Hisabati yatatokana na malengo ya
mwanafunzi yaliyowekwa katika Muhtasari wa somo la Hisabati kwa
shule za msingi kuanzia Darasa la III hadi la VII wa mwaka 2019. Aidha, umahiri uliotajwa katika muhtasari wa mwaka 2019 ndio utakaotahiniwa ili kubaini umahiri aliopata mwanafunzi katika miaka saba ya elimu ya msingi.

Fomati hii ni zao la maboresho yaliyofanyika kutoka fomati ya mwaka
2020 ambayo ilikuwa na maswali 45. Fomati iliyoboreshwa ina maswali
nane (8) yenye jumla ya vipengele 33 ambayo yametoka katika aina zote nane (8) za umahiri mahususi zilizotokana na umahiri mkuu wa aina tatu. Lengo la maboresho haya ni kumwezesha mtahiniwa kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea
duniani kote na ujenzi wa msingi wa umahiri katika masomo ya sekondari na elimu ya juu.

  • MALENGO YA JUMLA
    Mtihani wa Hisabati unalenga kupima uwezo wa mwanafunzi katika:
  • Kujenga uwezo wa kufikiri kimantiki kwa mwanafunzi;
  • Kujenga udadisi na uwezo wa utatuzi wa matatizo;
  • Kuweka misingi muhimu ya matumizi ya teknolojia, mawasiliano, ufikiri na tafakuri;
  • Kujenga uwezo wa kuchambua na kuwasilisha taarifa;
  • Kukuza uelewa wa maumbo, vipimo na matumizi yake katika
    maisha; na
  • Kujenga uwezo wa kujiamini katika kutumia maarifa, stadi na
    mwelekeo wa kihisabati katika maisha ya kila siku.

UMAHIRI MKUU
Mtihani huu unalenga kupima umahiri wa mwanafunzi katika:

  • Kutumia lugha ya kihisabati kuwasilisha wazo au hoja katika
    maisha ya kila siku;
  • Kufikiri na kuhakiki katika maisha ya kila siku; na
  • Kutatua matatizo katika mazingira tofauti.

FOMATI MPYA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI PSLE 2024

MUUNDO WA MTIHANI
Mtihani wa somo la Hisabati utakuwa na karatasi moja (1) na utafanyika kwa muda wa saa 2:00 kwa watahiniwa wote isipokuwa watahiniwa wenye mahitaji maalum ambapo mtihani wao utafanyika kwa saa 2:40. Mtihani utakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali nane (8) yenye vipengele 33. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote yenye jumla ya alama 50.

Sehemu A itakuwa na swali moja (1) ambalo ni swali la kwanza lenye
vipengele 10 kutoka katika Umahiri Mahususi wa Matendo ya Kihisabati. Kila kipengele kitakuwa na alama moja (1) na hivyo, jumla ya alama katika sehemu hii zitakuwa 10.

Sehemu B itakuwa na maswali matano (5); swali la pili, la tatu, la nne,
la tano na la sita yenye jumla ya vipengele 18 vya mafumbo (Word
Problems) kutoka kwenye umahiri mahususi wa aina tano (5). Swali la
pili litakuwa na vipengele sita (6) kila kipengele alama moja (1), swali la
tatu, la nne, la tano na la sita yatakuwa na vipengele vitatu (3) kila moja na kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2). Hivyo, jumla ya alama katika sehemu hii itakuwa 30.

Sehemu C itakuwa na maswali mawili (2), swali la saba na la nane.
Swali la saba litakuwa na vipengele viwili (2) kutoka katika Umahiri
Mahsusi wa kutumia stadi za takwimu kuwasilisha taarifa mbalimbali na
swali la nane litakuwa na vipengele vitatu (3) kutoka katika umahiri wa
kutumia stadi za maumbo katika miktadha ya Hisabati. Kila kipengele
kitakuwa na alama mbili (2), hivyo kufanya jumla ya alama katika
sehemu hii kuwa 10.

UMAHIRI MAHUSUSI UTAKAOPIMWA
Umahiri mahususi utakaopimwa katika mtihahi huu ni kama ifuatavyo:

  • kutumia dhana ya namba kuwasiliana katika mazingira tofauti;
  • kutumia stadi za mpangilio kufumbua mafumbo katika maisha ya kila siku;
  • kutumia matendo ya namba ya kihisabati katika kutatua matatizo;
  • kutumia stadi ya uhusiano wa namba na vitu katika miktadha
    mbalimbali;
  • kutumia stadi za vipimo katika miktadha mbalimbali;
  • kutumia stadi za maumbo katika miktadha ya Hisabati;
  • kutumia stadi za aljebra katika maisha ya kila siku; na
  • kutumia stadi za takwimu kuwasilisha taarifa mbalimbali

SAYANSI NA TEKNOLOJIA
UTANGULIZI
Fomati ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi katika somo la Sayansi na Teknolojia imeandaliwa kwa kuzingatia Muhtasari wa somo hilo wa mwaka 2015 ulioanza kutumika 2017 (toleo la 2019). Muhtasari huo umebainisha Umahiri Mkuu na Umahiri Mahsusi ambao
mwanafunzi anatakiwa kuupata katika ngazi ya Elimu ya Msingi Darasa la III hadi VII. Hivyo, mtihani wa somo la Sayansi na Teknolojia utakaoandaliwa kwa kutumia fomati hii, utalenga kupima umahiri alioupata mtahiniwa kuanzia Darasa la III hadi VII.

Fomati hii ni zao la maboresho yaliyofanyika kutoka fomati ya mwaka
2020 ambayo ilikuwa na maswali 45. Hivyo, mtihani wa somo la Sayansi na Teknolojia utakuwa maswali nane (8) yenye jumla ya vipengele 35 kutoka katika umahiri mahususi wa aina tisa (9)
uliotokana na umahiri mkuu wa aina tatu (3). Lengo la maboresho haya ni kumwezesha mtahiniwa kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea duniani kote na ujenzi wa msingi wa umahiri katika masomo ya sekondari na elimu ya juu.

MALENGO YA JUMLA
Mtihani wa somo la Sayansi na Teknolojia unalenga kupima ni kwa
kiwango gani mtahiniwa anaweza:

  • Kukuza uelewa na kutumia maarifa, stadi na kuwa na mwelekeo wa kisayansi na teknolojia;
  • Kujenga uwezo wa kutumia sayansi na teknolojia katika kutatua
    matatizo katika maisha ya kila siku; na
  • Kukuza stadi za kutenda na kutumia vifaa mbalimbali vya
    teknolojia.

UMAHIRI MKUU
Mtihani utazingatia tathmini ya ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:

  • Kufanya uchunguzi na ugunduzi wa kisayansi na kiteknolojia;
  • Kufahamu Misingi ya Sayansi na Teknolojia; na
  • Kutunza afya na mazingira.

MUUNDO WA MTIHANI
Mtihani wa somo la Sayansi na Teknolojia utakuwa na karatasi moja
(1) na utafanyika kwa muda wa saa 1:30 kwa watahiniwa wote isipokuwa, kwa watahiniwa wenye mahitaji maalum ambapo mtihani wao utafanyika kwa saa 1:45. Mtihani utakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali nane (8) yenye vipengele 35. Mtihani wa
somo la Sayansi na Teknolojia utakuwa na jumla ya alama 50.

Sehemu A itakuwa na maswali matatu (3); swali la kwanza, la pili na
la tatu yenye jumla ya vipengele 20. Swali la kwanza litakuwa na vipengele 10 vya maswali ya kuchagua herufi ya jibu sahihi kati ya machaguo matano (A-E) aliyopewa. Swali la pili litakuwa na vipengele vitano (5) ambavyo vitamtaka mtahiniwa kuoanisha maswali yaliyopo
katika Orodha A na majibu yaliyopo katika Orodha B. Swali la tatu litakuwa na vipengele vitano (5) ambavyo vitamtaka mtahiniwa kukamilisha sentensi kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Kila kipengele kitakuwa na alama moja (1) na hivyo, kufanya jumla ya
alama katika sehemu hii kuwa 20.

Sehemu B itakuwa na maswali matatu (3), swali la nne na swali la tano yenye vipengele vitatu (3) kwa kila swali na swali la sita lenye vipengele vinne (4). Maswali yote katika sehemu hii yatakuwa ya kuandika majibu mafupi. Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2) na hivyo, kufanya jumla ya alama katika sehemu hii kuwa 20.

Sehemu C itakuwa na maswali mawili (2); swali la saba na la nane. Swali la saba litakuwa na vipengele vitatu (3) na swali la nane litakuwa na vipengele viwili (2). Maswali hayo yatahusisha picha/ michoro au dhana mbalimbali za kisayansi zinazopima stadi za
kukokotoa. Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2). Hivyo kufanya
jumla ya alama katika sehemu hii kuwa 10.

UMAHIRI UTAKAOTAHINIWA
Umahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa somo la Sayansi naTeknolojia ni kama ifuatavyo:

  • kuchunguza vitu vilivyopo katika mazingira;
  • kutambua aina anuai za nishati na matumizi yake;
  • kutambua nadharia za kisayansi na kiteknolojia;
  • kutumia TEHAMA;
  • kumudu stadi za kisayansi;
  • kufanya majaribio kwa usahihi;
  • kufuata kanuni za usafi ili kuwa na afya na mazingira bora;
  • kufuata kanuni za afya ili kujenga afya bora; na
  • kutambua mifumo mbalimbali ya mwili wa binadamu.

URAIA NA MAADILI
UTANGULIZI
Fomati hii ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi somo la Uraia na
Maadili inazingatia Muhtasari wa somo la Uraia na Maadili Elimu ya Msingi Darasa la III-VII wa mwaka 2015 ulioanza kutumika 2017 (toleo la 2019). Muhtasari huu unasisitiza ujenzi wa umahiri kwa mwanafunzi, ili kuishi katika maadili yanayokubalika na jamii. Pia, muhtasari umejikita katika kumjengea mwanafunzi tabia inayokubalika ya kuheshimu na kuithamini jamii, uwajibikaji, ustahimilivu, uadilifu pamoja na kudumisha amani.

Fomati hii ni zao la maboresho yaliyofanyika kutoka fomati ya mwaka
2020 ambayo ilikuwa na maswali 45. Hivyo, mtihani wa somo la Uraia na Maadili utakuwa na maswali sita (6) yenye jumla ya vipengele 35 kutoka katika umahiri mahususi wa aina ishirini (20) uliotokana na umahiri mkuu wa aina sita (6). Lengo ni kumwezesha mtahiniwa kumaliza Elimu ya Msingi akiwa na umahiri zaidi wa kufikiri,
kuchambua mambo na kutumia maarifa aliyoyapata katika mazingira yanayomzunguka ili aweze kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea duniani kote na ujenzi wa msingi wa umahiri katika masomo ya sekondari na elimu ya juu.

MALENGO YA JUMLA
Mtihani utapima ni kwa kiwango gani mtahiniwa anaweza:

  • Kuelewa asasi na taasisi za kisiasa na kijamii na kazi zake katika
    utawala wa kidemokrasia;
  • Kutafisiri, kuthamini na kuheshimu vitambulisho vya taifa letu,
    Katiba, muundo na uendeshaji wa Serikali;
  • Kuelewa misingi ya kidemokrasia katika shughuli za utawala na
    uongozi;
  • Kutambua wajibu wao, kuheshimu na kutetea haki za binadamu
    na usawa wa sheria;
  • Kuelewa na kushiriki katika shughuli za utawala, uongozi, ulinzi
    na usalama wa taifa katika jamii wanamoishi;
  • Kuwa wabunifu na kuweza kubaini na kuchambua matatizo ya
    kisiasa, kiuchumi na kijamii na kubuni mbinu za kuyatatuaKutambua tofauti baina ya watu zitokanazo na itikadi na hali zao na kujenga uvumilivu kuhusu tofauti hizo;
  • Kujenga moyo wa umoja wa kitaifa na ushirikiano baina ya jamii za Tanzania na jamii za mataifa mengine; na
  • Kuishi kwa kutumia Elimu ya masuala mtambuka.

UMAHIRI MKUU
Utahini kwa kutumia fomati hii utazingatia upimaji wa ujuzi na utendaji
wa mtahiniwa katika:

  • Kuheshimu jamii;
  • Kuithamini jamii;
  • Kuwa mwajibikaji;
  • Kuwa mstahimilivu;
  • Kuwa mwadilifu; na
  • Kudumisha amani na maelewano.

MUUNDO WA MTIHANI
Mtihani wa somo la Uraia na Maadili utakuwa na karatasi moja (1) na
utafanyika kwa muda wa saa 1:30 kwa watahiniwa wote isipokuwa, kwa watahiniwa wenye mahitaji maalum ambapo utafanyika kwa saa
1:45. Mtihani utakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali sita (6) yenye vipengele 35. Watahiniwa watatakiwa kujibu maswali yote katika kila sehemu. Mtihani huu utakuwa na jumla ya alama 50.

Sehemu A itakuwa na maswali matatu (3); Swali la kwanza, la pili na la tatu yenye jumla ya vipengele 20. Swali la kwanza litakuwa na vipengele 10 vya Kuchagua jibu sahihi kati ya machaguo matano (5) A-E. Kila kipengele kitakuwa na alama moja (1), hivyo, kufanya jumla
ya alama 10. Swali la pili litakuwa la kuoanisha lenye vipengele vitano (5). Kila kipengele kitakuwa na alama moja (1), hivyo, kufanya jumla ya alama tano (5). Swali la tatu litakuwa na vipengele vitano (5) vya kujaza nafasi iliyoachwa wazi. Kila kipengele kitakuwa na alama moja (1) na hivyo kufanya jumla ya alama tano (5). Hivyo, sehemu hii
itakuwa na jumla ya alama 20.

Sehemu B itakuwa na maswali mawili (2); swali la nne na la tano yenye vipengele vitano (5) kila moja. Swali la nne litakuwa na vipengele vitano (5) vya kukamilisha jedwali/mchoro au kupanga sentensi ili kuleta mantiki. Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2). na hivyo kufanya jumla ya alama 10. Swali la tano litakuwa na vipengele vitano (5) vya majibu mafupi. Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2) na hivyo kuwa na jumla ya alama 10. Hivyo, sehemu hii itakuwa na jumla ya alama 20.

Sehemu C itakuwa na swali moja (1) lenye vipengele vitano (5) vya kutafsiri picha/ramani, kusoma kifungu cha habari na kujibu maswali yatakayoulizwa kwa kuandika majibu mafupi au kuandika maelezo mafupi juu ya dhana au hoja. Kila kipengele kitakuwa na alama mbili (2). Hivyo, sehemu hii itakuwa na jumla ya alama 10.

UMAHIRI UTAKAOTAHINIWA
Umahiri utakaopimwa katika mtihani wa somo la Uraia na Maadili ni
kama ifuatavyo:

  • Kujipenda na kuwapenda watu wengine, kuipenda na kujivunia
    shule yake, na kupenda Tanzania kwa kuenzi tunu za nchi na
    asili yake;
  • Kujijali na kuwajali wengine, kutunza mazingira na kujenga
    uhusiano mwema na watu wengine katika jamii;
  • Kulinda rasilimali na maslahi ya nchi, kusimamia majukumu
    yanayomhusu nyumbani na shuleni, kutii sheria na kanuni katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, kuwa na nidhamu na
    kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya nyumbani na
    shuleni;
  • Kuvumilia katika maisha ya kila siku, kufikia malengo aliyojiwekea kwa kuwa na mtizamo chanya na kujifunza kwa kuchanganua mambo kiyakinifu;
  • Kuaminika katika jamii, kutimiza majukumu yake kwa uwazi na
    ukweli na kusimamia haki; na
  • Kuchangamana na watu wenye asili tofauti, kuheshimu tofauti za
    kiutamaduni na mitazamo miongoni mwa watu wa jamii tofauti na kujenga urafiki mwema na mataifa mengine.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD FOMATI MPYA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI PSLE 2024

Sheria ya baraza la mitihani tanzania, Mwongozo wa semina za maelekezo kwa wasimamizi wa mitihani pdf, Mitihani ya NECTA Darasa la Saba Fomu ya fbm2, Necta OMR sheet PDF, Mitihani ya NECTA na majibu yake Past Papers, Mwongozo wa usimamizi wa mitihani 2024, Sheria za mitihani.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , ,

Comments are closed.