FOMU ya Maombi ya NIDA kwa Raia wa Tanzania
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
FOMU ya Maombi ya NIDA kwa Raia wa Tanzania
FOMU ya Maombi ya NIDA kwa Raia wa Tanzania, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ina jukumu muhimu nchini Tanzania, kwani inasimamia usajili na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa raia wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi.
Fomu ya NIDA 1A ni fomu ya maombi ambayo mtu yeyote anayetaka kupata kitambulisho anatakiwa kujaza.
Fomu hii ni hatua ya kwanza na muhimu katika mchakato mzima wa kupata kitambulisho cha Taifa.
Kupitia kitambulisho cha taifa (Kitambulisho cha NIDA), raia wanaweza kupata huduma mbalimbali za serikali na zakijamii kwa urahisi zaidi, kama vile kusajili laini za simu, kufungua akaunti za benki, kupata hati za kusafiria, na hata kununua ardhi.
Aidha, kitambulisho cha taifa cha NIDA ni nyenzo muhimu katika kuimarisha usalama wa raia na taifa kwa ujumla, kwani inasaidia katika kutambua uhalali wa mtu na kuzuia vitendo vya uhalifu mtandaoni na mtaani.
Kupitia Makala hii utafahamu jinsi gani Fomu hii inajazwa na hatua zingine zote muhimu katika mchakato wa maombi ili kurahisisha mchakato huu kwa kila Mtanzania anayehitaji kitambulisho cha Taifa (NIDA)
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD FOMU YA MAOMBI YA NIDA
(FOMU HII IJAZWE NA RAIA WA TANZANIA KWA WINO MWEUSI)
Fomu hii ni muhimu kwa kila raia wa Tanzania anayetaka kupata au kusahihisha kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Taarifa zinazohitajika Wakati Kujaza Fomu ya NIDA
Hakikisha una taarifa hizi zote tayari kabla ya kuanza kujaza fomu ili kurahisisha mchakato na kuepuka makosa.
TAARIFA ZAKO BINAFSI
- Jina lakoa kwanza, la kati, na la Ukoo
- Majina yako mengine (kama yapo)
- Tarehe yako ya kuzaliwa
- Namba ya cheti cha kuzaliwa
- Mahali ulipozaliwa
- Jinsia
- Hali ya Ndoa
- Taarifa za Elimu (shule ya msingi, wilaya, mwaka wa kuhitimu)
- Kazi na jina la mwajiri (kama umeajiriwa) Pamoja na
- Namba yako ya Simu.
TAARIFA ZA WAZAZI WAKO
- Majina ya kwanza, ya kati, na ya Ukoo ya Baba yako na Mama yako.
- Tarehe za kuzaliwa za Baba na Mama
- Nchi walikozaliwa Baba na Mama
TAARIFA ZA URAIA WAKO
- Uraia (kuzaliwa, Kurithi, au Kujiandikisha)
- Namba ya cheti cha kujiiandikisha (kama ipo)
MAHALI UNAPOISHI
- Namba ya nyumba, jina la Mtaa/Kijiji/Shehia, Kitongoji au Barabara
- Mkoa, Wilaya, Kata/Nchi
- Sanduku lako la Posta kama lipo
ANUANI YAKO YA MAKAZI YA KUDUMU
- Mkoa, Wilaya, Kata/Kijiji/Mtaa/Shehia, Kitongoji au Barabara
- Nchi, Sanduku la Posta kama lipo.
KUMBUKUMBU ZAKO BINAFSI
- Namba ya kitambulisho cha Taifa cha Baba na Mama
- Namba ya Pasipoti
- Namba ya Leseni ya Udereva
- Namba ya kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
- Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) TRA/ZRB
- Namba ya Uanachama wa bima ya afya
- Aina ya mfuko wa hifadhi ya Jamii na namba ya uanachama
- Namba ya cheti cha elimu ya sekondari na sekondari ya juu
- Namba ya kujiandikisha kupiga kura (NEC/ZEC)
- Cheti cha kuzaliwa
- Cheti za elimu ya msingi,
- Pasi ya kusafiria (Pasipoti)
- Cheti cha Elimu ya sekondari (kidato cha iv na vi)
- leseni ya Udereva
- Kadi ya Bima ya afya
- Kadi ya mfuko wa hifadhi ya jamii
- Kadi ya mpiga Kura
- Nambari ya mlipa kodi (Tin Number)
- Kitambulisho cha mzanzibar mkazi
- Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa