FURSA za Ufadhili wa Kujiendeleza Kada ya Afya Samia Program 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
FURSA za Ufadhili wa Kujiendeleza Kada ya Afya Samia Program 2024/2025
FURSA za Ufadhili wa Kujiendeleza Kada ya Afya Samia Program 2024/2025, Fursa za Ufadhili wa Kujiendeleza Kada ya Afya Kupitia Samia Health Specialization Program 2024/2025.
TANGAZO LA UFADHILI WA KUJIENDELEZA KWA WATUMISHI WA UMMA KADA ZA AFYA KUPITIA ‘DKT SAMIA HEALTH SPECIALIZATION SCHOLARSHIP PROGRAM’ KWA MWAKA 2024/2025
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Afya nchini kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya
zikiwemo huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi hapa nchini.
Uwekezaji katika Sekta ya Afya kwenye ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kutoa huduma zabafya, ajira za wataalamu wa afya, ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi
unatakiwa kwenda sambamba na kuendeleza wataalamu wa afya ili waweze kutoa huduma bora za matibabu ikiwemo ya matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi kwa
wananchi.
Katika kufanikisha azma ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha
huduma za kibingwa na kibobezi nchini, Wizara ya Afya imejiwekea lengo la kusomesha wataalamu wapya wa afya wasiopungua 300 katika ngazi za ubingwa na ubingwa bobezi
kwa kila mwaka wa fedha kupitia Mpango wa Ufadhili unaojulikana kama Dkt Samia Health Specialisation Scholarship Program in Tanzania.
Hivyo, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya anawatangazia watumishi wote waliopata udahili wa kusoma masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani za afya kwa mwaka 2024/2025 kwamba Dirisha la Maombi ya Ufadhili wa Masomo kupitia Dkt Samia Health Specialization Scholarship Program 2024 limefunguliwa.
Wizara imeanza kupokea maombi ya ufadhili kuanzia tarehe 09/08/2024 hadi tarehe 31/08/2024. Maombi hayo yatawasilishwa kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia ‘link‘ iliyotolewa kwenye tangazo hili.
Maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yatakayowasilishwa kwa njia ya mfumo huo tu.
Hivyo, waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya tangazo hili wanapaswa kufuata utaratibu huu.
Wataalamu watakaopata ufadhili wa masomo kwa vyuo vya nje ya nchi watalipiwa ada ya mafunzo, posho ya kujikimu, nauli pamoja na posho ya utafiti.
Wataalamu watakaopata ufadhili masomo katika vyuo vya ndani ya nchi watalipiwa ada ya mafunzo na posho ya utafiti pindi mtaalamu husika atapokuwa kwenye kipindi cha
kufanya utafiti kama sehemu ya mafunzo yake.
Malipo ya posho ya utafiti na posho ya
kujikimu yatazingatia viwango vilivyopangwa na Wizara.
Vigezo vitakavyotumika kuwapata watakaofadhiliwa ni kama ifuatavyo: –
- Kuwasilishwa kwa maombi rasmi ya ufadhili kwa njia ya mfumo (Post-graduate Sponsorship Online Application System).
- Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania.
- Awe mtumishi wa Serikali.
- Awe ana barua ya udahili (admission letter) kutoka kwenye chuo kinachotambuliwa
na Serikali ndani au nje ya nchi. - Awe anakwenda kusoma masomo ya ubingwa (specialization) au ubingwa bobezi
(super-specialization). - Mwombaji awe ametimiza miaka mitatu tangu alipoajiriwa (barua ya ajira na kuthibitishwa kazini iambatishwe wakati wa maombi).
- Ufadhili utazingatia uhitaji unaotokana na uhaba wa taaluma/fani anayokwenda
kusoma mtumishi kwenye kituo husika. Kwa mantiki hiyo, kipaumbele cha kupata
ufadhili itategemea upungufu wa taaluma aliyoomba kwenda kusoma kwenye kituo
chake cha kazi. - Kipaumbele kitatolewa kwa:
a. Kuzingatia mpango wa mafunzo wa kusomesha wataalamu ulioandaliwa kwaajili ya kutoa huduma maalum za kibobezi kwenye hospitali za Rufaa za Kanda, Maalum na Taifa.
b. Wataalamu waliopendekezwa na Taasisi zao kwa ajili ya kusoma mafunzo maalumu ya kimkakati ya ‘seti”.
c. Watumishi wa Serikali ambao baada ya mafunzo watarudi kwenye vituo vyao vya awali au kupangiwa vituo vingine kulingana na uhitaji.
d. Waombaji waliodahiliwa katika fani ambazo ni za kipaumbele katika utoaji wa huduma za kibingwa.
Fani hizo ni kama ifuatavyo
- Occupational Therapy, Physiotherpary, Audiology, Speech and Language Pathology, Orthotics & Prothotics
- Psychiatry, Mental Health Nursing, Clinical Psychology Oncology, Oncology Nursing, Radiology
- Anaesthesiology, Crtical Care
- Anatomical Pathology, Haematology, Microbiology and Immunology
- Infectious Disease Control, Parasitology and Entomology, Epidemiology and Laboratory Management.
- Otorhinolaryngology,Oral-Maxilofacial Surgery, Dentistry, Orthodontics, Periodontics, Dermatovenereology,
viii. Paediatrics, Surgery, Emergency Medicine, Internal Medicine, Orthopaedics Surgery, Opthalmology, Obstetrics and Gynaecology - Critical/Intensive Care Nursing, Pediatric Nursing, Cardiovascular
Nursing, Nephrology Nursing, Cardiovascular Perfusion, Midwifery and Womens Health, Neonatal Nursing, - Clinical Pharmacy, Pharmaconvigilance, Pharmaceutical Management,
Pharmaceutical Quality Control, Pharmacoeconomics, Industrial
Pharmacy - Waombaji waliodahiliwa katika nyanja za ubingwa bobezi (super-specialities) zenye upungufu ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi pamoja na kuchochea
tiba utalii kwenye Hospitali Maalum, Kanda na Taifa. - Neurosurgery, Neurology, Neuroradiology, Neurology Pediatric Surgery
- Transplant Sciences (Bone Marrow Transplant, Cochlea Impant na Liver Transplant), Plastic & Reconstructive Surgery, Hip & Knee Replacement
- Interventional Radiology, Medical Imaging, Women Imaging
- Infertility, Embriyology , Feto-Maternal Medicine
- Gyne-oncology, Surgical Oncology
- Addiction Sciences,
- Cardiology, Angiology, Cardio-thoracic Surgery, Cadiovascular
Sciences, Pediatric Cardiology - Neonatology, Paediatric Anaesthesia, Critical Care, Pediatric
Nephrology, Paediatric Oncology, Pediatric Haemato-oncology,
Paediatric Dentistry, Geriatric, Adolescent and Paediatric Psychiatry - Urology, Nephrology, Rhinology, Rheumatology
- Endocrinology, Respiratory Medicine, Pulmunology, Gastroenterology, Otology
- Vaccinology, Immunology, Infectious Diseases
- Medical Education
- Waombaji waliodahiliwa katika taaluma za menejimenti na uendeshaji wa huduma za afya kwa mfano, Health Monitoring and Evaluation, Health Systems Management, Health Policy and Planning, Health Economics, Health Financing, Health Promotion and Health Laws.
Aidha, mwombaji atatakiwa awe ameambatisha nakala halisi za nyaraka zifuatazo wakati wa kufanya maombi: –
- Barua ya ruhusa kwenda masomoni kutoka kwa mwajiri wake.
- Barua ya udahili kutoka chuoni.
- Cheti cha taaluma cha sasa (current academic qualification).
- Cheti cha usajili na leseni hai kutoka kwenye Baraza la taaluma husika.
- Cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Maombi yote yawasilishwe kwa kutumia ‘link’ ifuatayo: https://esponsorship.moh.go.tz/
MUHIMU: Kama ilivyoelekezwa hapo juu, mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 31/08/2024.
Imetolewa na: –
KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA,
Mji wa Serikali Mtumba,
Barabara ya Afya,
S.L.P 743,
40478 DODOMA.
09/08/2024
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Fursa za Ufadhili wa Kujiendeleza Kada ya Afya Kupitia Samia Health Specialization Program 2024/2025., FURSA za Ufadhili wa Kujiendeleza Kada ya Afya Samia Program 2024/2025