KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

GAMONDI aulizia huduma ya Kiungo wa Simba

Filed in Usajili, Michezo by on 03/05/2024 0 Comments

GAMONDI aulizia huduma ya Kiungo wa Simba

GAMONDI aulizia huduma ya Kiungo wa Simba

GAMONDI aulizia huduma ya Kiungo wa Simba

GAMONDI aulizia huduma ya Kiungo wa Simba, Klabu ya Simba msimu huu imekuwa na kiwango ambacho hakiwafurahishi mashabiki wake lakini kuna wachezaji ambao wamekuwa vipenzi vya mashabiki na wanaamini kama wataendelea kuwepo msimu basi timu hiyo itafanya vizuri.

Moja ya majina yanayotajwa yanawakosha mashabiki wa timu hiyo, ni kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma ambaye kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha tangu asajiliwe akitokea Al Hilal ya Sudan kimemfanya aanze kuuliziwa huku timu nyingine zikianza kutuma ofa.

Hilo ndilo lililomfanya Kocha, Miguel Gamondi kuiulizia huduma yake kwa kile alichokifanya kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Chanzo kimesema kuwa Kocha Gamondi aliulizia huduma ya mchezaji huyo baada ya mchezo dhidi ya watani zao Simba na licha ya kushinda dabi mbili walizokutana msimu huu, jicho la kocha huyo raia wa Argentina lilimtazama Ngoma na kugundua anaweza akaongeza kitu kwenye kikosi cha Wananchi.

“Baada ya dabi Kocha wa Yanga aliulizia iwapo wataweza kumpata Ngoma ingawa yeye anasisitiza bado ni mchezaji wa Simba kwani ana mkataba wa mwaka mmoja,” kilisistiza chanzo hicho.

Pamoja na Gamondi pia timu kama Pyramids FC na Al Ahly za Misri, Raja Casablanca ya Morocco zinahitaji huduma za Kiungo hiyo kutokana na kiwango chake bora.

GAMONDI aulizia huduma ya Kiungo wa SimbaInasemekana kuwa baada ya Ngoma kufanya vizuri kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilipocheza dhidi ya Al Ahly, kocha wa timu hiyo, Marcel Koller hakusita kuanza mchakato wa kuhitaji huduma yake.

Ikumbukwe kuwa kiungo huyo aliwahi kuichezea Raja kabla ya kuamua kutimkia Kuwait kisha kutua Al Hilal ya Sudan na baadaye aliamua kuvunja mkataba kutokana na machafuko nchini humo na kujiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Alianza kuifungia Simba kwenye mchezo wa Simba Day dhidi ya Power Dynamo kwenye ushindi wa mabao 2-0, huku bao jingine likifungwa Willy Esomba Onana.

Kwenye Ligi Kuu Bara Ngoja amefunga mabao mawili lakini ameonyesha ubora kiungo ya kati na kuwakosha mashabiki na makocha ambao wanatamani kufanya nao kazi.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *