HERSI Athibitisha Aziz Ki Hajasaini Mkataba Mpya
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
HERSI Athibitisha Aziz Ki Hajasaini Mkataba Mpya
HERSI Athibitisha Aziz Ki Hajasaini Mkataba Mpya,Rais wa klabu ya Yanga Sc Engineer Hersi Said amethibitisha kuwa kiungo Mshambuliaji Stephanie Aziz Ki bado hajasaini nyongeza ya mkataba mpya klabuni hapo na kubainisha kuwa mazungumzo bado yanaendelea lakini hakuna kilichokamilika baina ya pande hizo mbili.
Akizungumza na Soccer Laduma, Eng. Hersi amesema kuwa klabu ya Yanga ipo kwenye wakati mgumu kumpoteza mchezaji kama Azizi Ki huku akasisitiza kuwa hajamaanisha wanakwenda kumpoteza Azizi Ki.
“Unajua tulimsajili kwa mkataba wa miaka miwili na huo mkataba umeisha na hiyo ina maana wanaomtaka wanazungumza naye moja kwa moja. Lakini kwa upande wetu bado tunazungumza naye na hakuna kilichokamilika.” Eng. Hersi
Eng. Hersi amekiri kuwa Azizi Ki ana ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali zikijumuisha baadhi ya klabu kutoka Afrika Kusini lakini amewatoa hofu Wananchi kuwa klabu hiyo ina uhusiano imara sana na mchezaji huyo na wamelifanyia kazi jambo hili kama viongozi kuhakikisha kuwa anabaki.