HERSI Aziz Ki bado yupo sana
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
HERSI Aziz Ki bado yupo sana
HERSI Aziz Ki bado yupo sana, Rais wa Yanga, Hersi Said amewahakikishia Wanachama wa Klabu hiyo kuwa, Mchezaji wao Stephen Aziz Ki bado yupo sana katika timu yao mpaka pale ambapo Yanga itatimiza malengo yake ya kuwa klabu Bora zaidi Barani Afrika.
“Aziz Ki bado yupo sana kwani hajamaliza kazi iliyomleta Tanzania. Ataondoka nchini pale atakapomaliza kazi hiyo,” alisema Hersi na kuibua shwangwe kwa mashabiki
Aziz Ki mwenyewe aliwahi kutoa kauli kama hiyo kuwa kilichomleta Yanga ni kushinda Makombe lengo likiwa Ligi ya Mabingwa na kazi hiyo bado hajaitimiza hivyo pale atakapoisaidia Yanga kucheza fainali na hata kubeba taji la Ligi ya Mabingwa basi ndipo ataondoka
“Mpaka sasa Mimi ni Mchezaji wa Yanga na nafasi kubwa zaidi nawapa Yanga, namwamini Rais wa Yanga @caamil_88 yeye ndiye amenileta hapa, tuna makubaliano yetu mimi na yeye kuwa Yanga inapaswa kucheza Fainali ya Afrika na tutwae kikombe, hiyo ndio ndoto yangu na ikitokea tumecheza Fainali na kubeba Ubingwa nitamfuata Rais kumwomba Baraka zake ili niondoke zangu, ila kwasasa bado malengo yangu na Yanga hayajatimia mpaka tucheze fainali ya Afrika”
-Stephen Aziz Ki wa Yanga, akijibu swali la Mwandishi Zainab Mohamed wa TvAyoma kama atasalia Yanga msimu ujao wa 2024/2025.