KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

HERSI Said aeleza Jinsi alivyomsajili Aziz Ki

Filed in Michezo by on 29/04/2024 0 Comments

HERSI Said aeleza Jinsi alivyomsajili Aziz Ki

HERSI Said aeleza Jinsi alivyomsajili Aziz Ki

HERSI Said aeleza Jinsi alivyomsajili Aziz Ki

HERSI Said aeleza Jinsi alivyomsajili Aziz Ki, Rais wa Klabu ya Young Africans Hersi Said ameeleza njia alizotumia kuinasa saini ya Kiungo Mshambuliaji Kutoka Burkina Faso, Stephen Aziz Ki.

Hersi ameeleza kuwa alisafiri hadi Morocco kwaajili ya kumuona Aziz Ki na ndipo urafiki na mawasiliano vilianza hadi kukamilisha dili lake la kutua Kwa Wananchi.

Hersi ameeleza kuwa;

“Story ya Aziz ilianza muda mrefu, wakati huo Yanga haishiriki katika michuano ya kimataifa lakini Simba wako kimataifa na walikuwa group moja na ASEC Mimosas na Aziz akaja kucheza hapa Dar akafunga, Aziz akawa anatajwa sana na wakati anatajwa alitajwa kwa muktadha wa kwenda Simba.

“Unawezaje kumshawishi mchezaji ambaye anashiriki michuano ya kimataifa kuja kucheza kwenye timu ambayo haina rekodi ya kufanya vizuri kimataifa ?.

HERSI Said aeleza Jinsi alivyomsajili Aziz Ki“Nilianza kumfuatilia Aziz nikatafuta namba zake nikazipata, nilishawahi kufunga safari hapa nikaenda mpaka Berkane, Morocco kwaajili ya kwenda kumuona Aziz akicheza kukutana nae na kujenga urafiki.

“Baada ya ile mechi kati ya Berkane na Asec nilienda hadi hoteli ya kina Aziz, wakati naongea nao nikajiiba nikaingia kwenye chumba cha Aziz Ki tukazungumza nikamwambia nina interest na wewe akaniambia umesafiri kutoka Tanzania hadi hapa kwaajili yangu ? Nikamwambia ndio, palepale nikapata na namba ya Mama yake.

Nikaanza kuwasiliana na Mama yake nikamwambia namtaka kijana wako nikaenda tena Ivory Coast nikapeleka Ofa yangu, ofa yangu ilikuwa ndogo kuliko ofa ambayo klabu za Sudan na Tanzania walikuwa wamepeleka kwa Aziz hapo sasa ndio tukaanza kuongea nikamwambia Mama Aziz nitamtunza Aziz kama mzazi,” Rais wa Yanga Sc, Mhandisi, Hersi Said akizungumza kwenye kipindi cha Bao la asubuhi cha Bongo Fm.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *