HESBL Yakanusha Kadi ya Uanachama kuwa Sifa ya Kupata Mkopo
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
HESBL Yakanusha Kadi ya Uanachama kuwa Sifa ya Kupata Mkopo
HESBL Yakanusha Kadi ya Uanachama kuwa Sifa ya Kupata Mkopo,Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL) imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii, kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoomba mkopo wanapaswa kuwa na kadi za chama cha siasa ili kupata mikopo.
Upangaji mikopo ya Elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) unaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) na miongozo ambayo hutolewa kila mwaka kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili na kupatikana katika www.heslb.go.tz
Sifa zinazotajwa na Sheria na miongozo ni mwombaji.
- Awe Mtanzania; Awe ameomba mkopo
- Awe amepata udahili katika taasisi inayotambuliwa na mamlaka za Serikali;
- Asiwe na chanzo kingine cha fedha cha kugharamia masomo; na kwa anayeendelea na masomo,
- awe amefaulu mitihani ya mwaka uliotangulia.
Aidha, miongozo inatoa kipaumbele kwa wahitaji kutoka katika makundi maalum kama yatima, wenye ulemavu na waliofadhiliwa katika masomo yao ya sekondari au stashahada ambao hupaswa kuthibitisha uhitaji wao kwa kujaza fomu maalum wakati wa uombaji.
Hivyo, miongozo ya mwaka wa masomo 2024/2025, kama ambavyo imekuwa katika miongozo ya miaka iliyopita, haitaji sifa ya uanachama kwa chama cha siasa kama kigezo cha kupata mkopo wa elimu ya juu.
Kwa msingi huo, Bodi inawashauri wanafunzi wote wanaoomba mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB KUSOMA na KUZINGATIA miongozo ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, siku ya Jumatatu, Mei 27, 2024 jijini Tanga na ambayo inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).
- HESLB Muongozo wa Maombi ya Mikopo 2024/2025
- IFAHAMU Miongozo ya Utoaji Mikopo iliyozinduliwa 2024/2025
- MIONGOZO ya Samia Scholarship 2024/2025
- WANAFUNZI Kaya Maskini Kupata Mkopo Elimu ya Juu Asilimia 100
- MUONGOZO wa Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo kwa Mfumo wa Kidijitali ERITA
- NACTE Muongozo wa Maombi ya Vyuo Certificate na Diploma 2024/2025
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: HESBL Yakanusha Kadi ya Uanachama kuwa Sifa ya Kupata Mkopo