HESBL Yaongeza Muda wa Maombi ya Mikopo 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL) inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo umeongezwa mbele hadi tarehe 14 Septemba, 2024.
Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa.
Itakumbukwa kuwa, awali Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao tarehe 1 Juni, 2024 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 31 Agosti, 2024.
Kupitia tangazo hili, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 ambao hawajakamilisha maombi yao wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.
Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2024.
Soma na hizi:
- HESBL Taarifa Muhimu kwa Wanafunzi wa Stashahada (Diploma)
- HESBL Jinsi ya Kuomba Mkopo 2024/2025
- KOZI Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB
- HESLB Muongozo wa Maombi ya Mikopo 2024/2025