HESLB Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Wanaoomba Mikopo 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
HESLB Maelekezo Muhimu kwa
Wanafunzi Wanaoomba
Mikopo 2024/2025
HESLB Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Wanaoomba Mikopo 2024/2025,dirisha la mkopo 2024/2025, HESLB login,Wanafunzi Waliopata Mkopo, Mwongozo wa kuomba mkopo diploma,HESLB news today,mwongozo wa utoaji mikopo 2024/2025.
Waombaji wote wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2024/2025
wanafahamishwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
- Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo wa mwaka wa masomo 2024/2025.
- Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa Kidato cha Nne atakayoitumia mwombaji iwe sawa kwenye maombi ya mkopo na udahili wa chuo.
- Waombaji ambao wamefanya mtihani wa Kidato cha Nne zaidi ya mara moja wahakikishe wanaorodhesha namba zote za mtihani katika maombi yao.
- Kuhakikisha kuwa nyaraka zote za maombi ya mkopo anazowasilisha
mwombaji ziwe zimehakikiwa na mamlaka husika. - Kuhakikisha kwamba vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii
Zanzibar (ZCSRA) au Afisa aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo. - Kuhakikisha wanafunzi waliozaliwa nje ya nchi au wanafunzi ambao wazazi
wao wamefariki dunia wakiwa nje ya nchi wanaambatanisha barua za uthibitisho kutoka RITA au ZCSRA. - Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao.
- Kila mwombaji ahakikishe taarifa zake za benki zimejazwa kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo.
- Taarifa hizo ndizo zitakazotumika kumlipa mwanafunzi mkopo wake kipindi atakachokuwa masomoni. hivyo hazitaruhusiwa kubadilishwa bila HESLB kujulishwa rasmi;
- Namba ya simu ya mkononi ya mwombaji itakayotumika wakati wa kusajili maombi ya mkopo ndiyo itakayotumika kumtaarifu hatua mbalimbali za maombi
yake. - Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.
Soma zaidi HESLB Muongozo wa Maombi ya Mikopo 2024/2025
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: dirisha la mkopo 2024/2025, HESLB login, HESLB Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Wanaoomba Mikopo 2024/2025, HESLB news today, Mwongozo wa kuomba mkopo diploma, mwongozo wa utoaji mikopo 2024/2025., Wanafunzi Waliopata Mkopo