SELECTION ZA FORM FIVE NA VYUO VYA KATI 2024 BONYEZA HAPA


MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BONYEZA HAPA


RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2023/2024 BONYEZA HAPA


JINSI YA KUANGALIA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA FORM FIVE 2024 BONYEZA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA


HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma

Filed in Ajira, Michezo by on 21/12/2023 0 Comments

HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma

HESLB Fahamu Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma,VIGEZO na Sifa za Kupata Mkopo HESLB 2023/2024, HESLB Muongozo Na Sifa za Kupata Mkopo 2023/2024,Vigezo Na Sifa Za Kupata Mkopo Elimu Ya Juu 2023/2024 (HESLB),FAQss Maswali Kuhusu Utoaji Wa Mikopo, mambo muhimu ya kuzingatia kwa waombaji mkopo kwa 2023/2024, maelezo ya awali kwa waombaji mikopo kwa mwaka 2023/2024,HESLB mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku 2022/2023, BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU 2023-2024|SIFA ZA KUPATA MKOPO 2023/24| TAARIFA KWA UMMA HESLB - YouTube,HESLB – Vigezo vya Kuomba mkopo wa Elimu ya juu,Mwongozo Wa Maombi Ya Mkopo 2023/2024 HESLB Guidelines,HESLB – Vigezo vya Kuomba mkopo wa Elimu ya juu,Gpa ya kupata mkopo,HESLB login,Dirisha la Mkopo 2023/2024,Vigezo vya kupata mkopo heslb,vigezo vya kupata mkopo ngazi ya diploma 2023/2024,Vigezo vya kupata mkopo ngazi ya diploma PDF.

HESLB Fahamu Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma

HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma, HESLB Fahamu Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma,HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma, Sifa za Kupata Mkopo Diploma, vigezo vya kupata mkopo vyuo vya kati,vigezo vya kupata mkopo nmb,vigezo vya kupata mkopo ngazi ya diploma pdf,HESLB – Vigezo vya Kuomba mkopo wa Elimu ya juu.

Heslb Vigezo Vya Kupata Mkopo To apply for a loan from the Higher Education Students’ Loans Board (HESLB) in Tanzania, there are certain qualifications and requirements that must be met. HESLB is a government institution established to provide loans and scholarships to Tanzanian students pursuing higher education.

HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma

VIGEZO na Sifa za Kupata Mkopo HESLB 2023/2024, Vigezo Na Sifa za Kupata Mkopo 2023/2024 ,Sifa na Vigezo Kupata Mkopo HESLB 2023,Jinsi ya Ku apply Mkopo HESLB 2023,Muongozo wa Mikopo 2023,HESLB Kitabu cha Muongozo PDF 2023,HESLB Loan Guidelines 2023/2024

Waombaji wote wa mikopo watarajiwa mnasisitizwa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo pamoja na taratibu nyingine za uombaji mkopo kabla ya kujaza fomu za maombi ya mkopo zinazopatikana kwenye mtandao wa https://olas.heslb.go.tz

MAELEKEZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WANAOOMBA MIKOPO

Waombaji wote wa mikopo ya
elimu kwa ngazi ya Stashahada kwa mwaka wa masomo 2023/2024
wanafahamishwa kuzingatia mambo
yafuatayo:-

(i) Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo
wa mwaka wa masomo 2023/2024;
(ii) Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne atakayoitumia mwombaji iwe sawa na aliyoombea udahili wa chuo;
(iii) Kuhakikisha kuwa fomu ya maombi ya mkopo na mkataba zimesainiwa na viongozi wa serikali ya mtaa, mdhamini na kamishna wa viapo.;
(iv) Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao;
(v) Kuhakikisha kwamba vyeti vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa
na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa
aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo;
(vi) Kwa mwombaji mwenye akaunti ya benki ajaze taarifa zake kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo;
(vii) Kwa mwombaji mwenye Namba ya simu na kitambulisho cha taifa (NIDA) ahakikishe anajaza namba hizo wakati wa kuomba mkopo.
(viii) Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao

KUFUNGULIWA DIRISHA LA MAOMBI AWAMU YA PILI

Kwa wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu kwa ngazi ya Stashahada kwa awamu ya pili, dirisha la maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 limefunguliwa kwa siku 14 kuanzia tarehe 21 Disemba, 2023 hadi tarehe 04 Januari, 2024.

Dirisha la awamu ya pili, wanafunzi walengwa wamegawanyika katika
makundi matatu ambao watapaswa kuwasilisha maombi yao kwa
njia ya mtandao kupitia https://olas.heslb.go.tz

Kundi la Kwanza ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Stashahada
za kipaumbele kama zilivyotajwa katika ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’ ambao awali hawakuweza kuomba kwa
sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa hadi dirisha kufungwa.

Kundi la Pili ni wanafunzi wa mwaka wa pili au wa tatu wa Stashahada za kipaumbele kama zilivyotajwa katika ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’. Wanafunzi hawa, ambao awali hawakuweza kuomba mkopo, sasa wanaruhusiwa kuomba.

Kundi la Tatu ni wanafunzi wa Stashahada za kipaumbele
ZILIZOONGEZWA kupitia mwongozo huu; ‘TOLEO LA PILI’ la ‘Mwongozo
wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka
2023-2024’.

Wanafunzi wote wanaoomba mkopo wa Stashahada kupitia dirisha hili la awamu ya pili wanakumbushwa kusoma ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’ ambao unapatikana katika www.heslb.go.tz na www.nactvet.go.tz

SIFA STAHIKI

VIGEZO VYA MSINGI VYA MWOMBAJI MKOPO

Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo zinaainisha sifa na vigezo vya jumla kwa wanafunzi wanaohitaji mkopo baada ya
kudahiliwa na vyuo vyenye ithibati.

Mwombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

(i) Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 27 wakati wa kuomba mkopo;
(ii) Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu ya ngazi ya kati nchini;
(iii) Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);
(iv) Asiwe na ajira au mkataba wa kazi wa serikalini au sekta binafsi unaompatia mshahara au kipato;
(v) Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (CSEE), Cheti (astashahada) au kidato cha sita (ACSEE) au ndani ya
miaka mitano; yaani kati ya mwaka 2019 hadi 2023.

HALI YA KIJAMII NA KIUCHUMI

(i) Uyatima; aliyefiwa na mzazi au wazazi
(ii) Familia au kaya ya kipato duni inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za
kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni;
(iii) Ulemavu wa mwombaji au wazazi wake.

UPANGAJI WA MIKOPO

Upangaji wa mikopo utazingatia
vipaumbele vifuatavyo:-

(i) Mwanafunzi mwenye udahili kwenye
programu za vipaumbele vya Taifa
kama zilivyofafanuliwa katika Kipengele
cha 6 cha Mwongozo huu zitazingatiwa;
(ii) Ufaulu wa kitaaluma uliomuwezesha
kudahiliwa kwa ajili ya elimu ya ngazi ya kati; na
(iii) Hali ya kijamii kama  livyofafanuliwa katika kipengele cha 3.2 cha mwongozo huu.

NYARAKA ZA KUAMBATISHA WAKATI
WA MAOMBI YA MKOPO

(i) Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
(ii) Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar
au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
(iii) Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji au mzazi iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mkoa (RMO);
(iv) Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mzazi wa mwombaji iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
(v) Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

MAENEO NA PROGRAMU ZA
KIPAUMBELE KATIKA UTOAJI WA MIKOPO

MAENEO YA KIPAUMBELE

Mkopo utatolewa katika maeneo makuu sita yakiakisi vipaumbele vya Taifa kama ilivyoainishwa katika tangazo la Serikali Namba 715 la tarehe 29 Septemba 2023.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-
(i) ‘Health & Allied Sciences’;
(ii) ‘Education and Teaching’;
(iii) ‘Transport & Logistics’;
(iv) ‘Energy Engineering’;
(v) ‘Mining & Earth Science’ and
(vi) ‘Agriculture & livestock’

PROGRAMU ZA KIPAUMBELE
Katika mwaka wa masomo 2023/2024 mikopo itatolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Program/Stashahada zinazoangukia/zilizomo katika maeneo sita ya kipaumbele yaliyoidhinishwa – rejea kipengele 6.

AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI
(HEALTH & ALLIED SCIENCES)

Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Clinical Dentistry’;
(ii) ‘Diagnostic Radiotherapy’;
(iii) ‘Occupational Therapy’;
(iv) ‘Physiotherapy’;
(v) ‘Clinical optometry’;
(vi) ‘Dental Laboratory technology’;
(vii) ‘Orthotics & Prosthetics’;
(viii) ‘Health record & information; and
(ix) ‘Electrical and Biomedical Engineering’

ELIMU YA UALIMU (EDUCATION AND TEACHING)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUTAZO:-
(i) Diploma in Education (Physics and
Mathematics); and
(ii) Diploma in Teaching (Technical and
Vocational Education).

USAFIRI NA USAFIRISHAJI (‘TRANSPORT AND LOGISTICS’)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUATAZO:-
(i) ‘Aircraft Mechanics’;
(ii) ‘Shipbuilding and repair’;
(iii) ‘Railway construction and maintenance;
(iv) ‘Global Logistics and Supply Chain
Management’,
(v) ‘Marine Trasport and Nautical Science’,
(vi) ‘Shipping and Logistics Management’, and
(vii) ‘Transport and Supply Chain Management’.

UHANDISI WA NISHATI (‘ENERGY ENGINEERING’)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUATAZO:-
(i) ‘Renewable Energy Engineering
(Hydro, Wind, Solar)’;
(ii) ‘Pipeline, Oil and Gas Engineering’,
(iii) ‘Oil and Gas Engineering Technology’,
(iv) Environmental Engineering and
Management’,
(v) ‘Naval Architecture and Offshore
Engineering’,
(vi) ‘Metallurgy and Mineral Processing
Engineering’, and
(vii) ‘Mining Engineering’.

MADINI NA SAYANSI YA ARDHI
(‘MINING AND EARTH SCIENCE’)

Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Lapidary and Jewelry’;
(ii) ‘Mineral Processing’,
(iii) “Geology and Mineral Exploration’,
(iv) ‘Petroleum Geosciences and Exploration’,
and
(v) ‘Land and Mine Surveying’.

KILIMO NA UFUGAJI (‘AGRICULTURE AND LIVESTOCK)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUATAZO:-
(i) ‘Leather Technology’;
(ii) ‘Food Technology and Human Nutrition’;
(iii) ‘Sugar Production Technology’;
(iv) ‘Veterinary Laboratory Technology’;
(v) ‘Horticulture’;
(vi) ‘Irrigation Engineering’;
(vii) ‘Agro Mechanization’,
(viii) ‘Range Land Management and Tsetse fly
control from Livestock”, and
(ix) ‘Sugarcane Production Technology’.

VIPENGELE NA VIWANGO VYA MKOPO

Waombaji watakaopangiwa mikopo watapangiwa viwango vya fedha
kulingana na mahitaji halisi ya vyuoni.

Mkopo utagawanywa katika vipengele vya mkopo kwa mtiririko ufuatao: Chakula na Malazi, Ada ya Mafunzo, Gharama za Vitabu na viandikwa, Mahitaji maalumu ya Kitivo,
Gharama za Utafiti na Mafunzo kwa Vitendo.

Mkopo utatolewa kwaajili ya kugharamia vipengele vyote au baadhi ya vipengele, kama itakavyochambuliwa na kuidhinishwa.

CHAKULA NA MALAZI

Kiwango cha juu kisichozidi TZS. 7,500.00 kwa siku kitatolewa kulingana na idadi ya siku mwanafunzi atakuwa chuoni kama inavyoelekezwa kwenye kalenda ya chuo husika. Kiasi hiki kitalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi.

ADA YA MAFUNZO

Kiwango cha juu cha ada kisichozidi TZS. 1,400,000.00 kwa mwaka kulingana na gharama zinazolipwa katika chuo husika kwa mwaka na kitalipwa moja kwa moja kwa chuo husika.

GHARAMA ZA VITABU NA VIANDIKWA

Kiwango cha juu cha kisichozidi TZS. 200,000.00 kwa mwaka kwa
vitabu na viandikwa na kitatolewa kwa wanafunzi.

MAHITAJI MAALUMU YA KITIVO

Kiwango cha juu kisichozidi TZS. 300,000.00 kwa mwaka kulingana
na gharama husika zitalipwa moja kwa moja chuoni.

MAFUNZO KWA VITENDO

Kiwango cha juu kisichozidi TZS. 7,500.00 kwa siku hadi siku 56 kwa
mwaka, kwa ajili ya Mafunzo kwa Vitendo kitatolewa.

Kiasi hicho kitalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi.

GHARAMA ZA KAZIMRADI

Kiasi kisichozidi TZS. 100,000.00 kwa mwaka kitatolewa kwa gharama za kazimradi kwa baadhi ya programu kama zilivyoainishwa na chuo husika.

MASHARTI MENGINE

WAJIBU WA MDHAMINI NA MZAZI/MLEZI

Wazazi/Walezi na wadhamini wana wajibu wa kuthibitisha usahihi wa taarifa ambazo zitawasilishwa katika fomu ya maombi ya mkopo kabla ya kusaini. Mdhamini/Mzazi atatakiwa kuhakikisha kwamba mkopaji anajaza taarifa sahihi zitakazotumika wakati wa urejeshaji.

Aidha mdhamini
atatakiwa kutoa taarifa za mkopaji na makazi pale atakapochelewa au kushindwa kurejesha mkopo wake.

Kwa mwanafunzi alie na umri chini ya miaka 18 wakati wa kuomba mkopo atalazimika kujaza tamko rasmi
(declaration) kuridhia kuendelea kupokea mkopo pindi atakapotimiza umri wa miaka 18.

Mwombaji wa mkopo anapaswa kuambatanisha picha (passport size) ya mdhamini na nakala ya kitambulisho
kimojawapo kati ya vilivyotajwa hapo chini ambacho kimetolewa na mamlaka za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:-

(i) Kitambulisho cha Taifa
(ii) Kadi ya mpiga kura
(iii) Leseni ya udereva
(iv) Pasi ya kusafiria
(v) Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi

UREJESHAJI MKOPO
Baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya kati, mnufaika wa mkopo atatakiwa kurejesha mkopo wake wote kwa
makato yasiyopungua asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara wake wa kila mwezi au kiwango kisichopungua TZS 100,000.00 kwa mwezi kwa Mnufaika
aliyejiajiri kwenye sekta isiyo rasmi.

Iwapo mnufaika ataachishwa/atakatisha masomo, mkopo huo wote utalipwa kwa mkupuo.

Mikopo yote inatozwa asilimia
moja (1%) ya ada ya uendeshaji kwenye deni la msingi la mnufaika kwa mara moja.

HESLB Online Application 2023/2024 – OLAMS Login | Register 2023/24,OLAMS Login HESLB – Tanzania HESLB Login 2023/2024,HESLB Online Loan Application (OLAMS) 2023/2024,HESLB Loan Application 2023/2024,HESLB OLAMS Online Loan Application 2023/2024, OLAMS Login 2023/2024, OLAMS Register 2023/2024, How do I check my Heslb loan allocation?,How can I view my Heslb loan allocation?, What is the application fee for Heslb loan?, How do I log into my Heslb account?HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma, HESLB Fahamu Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma,HESLB Vigezo na Sifa za Kupata Mkopo Diploma, Sifa za Kupata Mkopo Diploma, vigezo vya kupata mkopo vyuo vya kati,vigezo vya kupata mkopo nmb,vigezo vya kupata mkopo ngazi ya diploma pdf,HESLB – Vigezo vya Kuomba mkopo wa Elimu ya juu.

fomu ya kuomba mkopo, Vigezo vya kupata mkopo pdf, Vigezo vya kupata mkopo CRDB Bank, Vigezo vya kupata mkopo nmb, vigezo vya kupata mkopo ngazi ya diploma 2023/2024, Vigezo vya kupata mkopo vyuo vya kati, Vigezo vya Kupata Mkopo 2024/2025, Gpa ya kupata mkopo, Fomu Ya Kuomba Mkopo, Fomu Ya Kuomba Mkopo HESLB, Jinsi ya kuomba mkopo Online, Jinsi ya Kuomba Mkopo wa Elimu ya Juu, MFANO Wa Fomu Ya Mkopo HESLB PDF.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

KUPATA NIDA BURE BONYEZA HAPA

KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA

KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA

KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

Tags: , , , , , , , , , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *