RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

Historia ya Yanga SC 1935

Filed in Michezo, Makala by on 01/12/2023 0 Comments

Historia ya Yanga SC 1935

Historia ya Yanga SC 1935

Historia ya Yanga SC 1935

Historia ya Klabu ya Yanga SC inatokea tangu enzi za miaka ya 1910, ingawaje historia kamili ilianza kuandikwa mwaka 1935.

Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs ambayo Mwaka 1935 uwezo wake ulishuka sana kusababisha wanachama kutofautiana na kuleta migogoro katika Klabu na ukasababisha baadhi ya wanachama kujiengua na kuanzisha Klabu nyingine baada ya New Young’s kushuka Daraja.

Wanachama walioondoka waliunda Klabu iliyojulikana kwa jina la Queens FC. ambayoa baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Sunderland ambayo kwa sasa inajuliakana kama Simba SC.

Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs vijana wa Dar es Salaam walikuwa na desturi ya kukutana viwanja wa Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani Boys.

Ndani ya kipindi kifupi timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo, miongoni mwao waliovutiwa na uanachama wa klabu hiyo ni Tabu Mangala (Sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926 walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi sasa kuna shule ya sekondari ya Tambaza.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo bandarini.

Baada ya mkutano huo, timu ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana wa Jangwani hao.

IFAHAMU Historia ya Yanga SC (Young Africans SC)

Enzi hizo kikosi cha Yanga cha ushindani kikiwa uwanjani tayari kwa mchezo

Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wanatembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani wao, kwamba katika kipindi hicho wao ndiyo zaidi, kwa sababu Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Italiana.

Taliana FC ilipata mafanikio ya halaka na haikushangaza ilipopanda ligi Daraja la pili kanda ya Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930 Taliana waliamua kuachana nalo mapema kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.

Kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu vipya pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs waliweza kutwaa kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.

Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs 1935 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland kutokana na New Youngs kushuka Daraja.

Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.

Miaka ya 80 baadaye leo, ni timu ya kihistoria Tanzania ikiwa inaongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa mara 27.

Pongezi nyingi ziwaendee wachezaji wote waliopata kuichezea timu hiyo kuanzia enzi za Jangwani Boys, Navigation, Italiana, New Youngs hadi leo hii ikijulikana kama Yanga SC ingawa katika cheti chake cha usajili inafahamika kama Dar Young Africans.

Historia ya Yanga SC 1935

Historia ya Yanga SC 1935

Mafanikio ya Yanga ndani ya miaka 80 hayakuja hivi hivi bila kuwapongeza viongozi ambao waliihangaikia timu hiyo inasimama kidete, viongozi wa enzi hizo hadi leo hii wanastahili pongezi kwa kuiwezesha kutwaa mara nyingi ubingwa wa nchi.

IFAHAMU Historia ya Yanga SC (Young Africans SC)Wachezaji wa zamani wa Yanga ambao kwa sasa wameunda timu yao ya Yanga veterani

Shukrani nyingine ziwaendee wanachama, wapenzi na mashabiki, bila kuwasahau waandishi wa habari, bila hamasa zao sidhani kama Yanga ingeweza kufika hapo ilipo, hiyo ndivyo historia ya klabu ya Yanga ambayo ndio iliyozaa Sunderland leo hii ikiitwa Simba SC.

Yanga imetoa viongozi mbalimbali wa soka na serikali mmoja wapo ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye mwaka 1976 alipokuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo na kuwezesha usajili wa Shaaban Katwila.

Pia Yanga imetoa rais wa CECAFA Leodegar Tenga, rais wa TFF Jamal Malinzi, nahodha wa Taifa Stars na Zanzibar Heroes Hadir Haroub ‘Cannavaro’na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa na wengineo.

Yanga imekuwa na mafanikio makubwa sana tangu kuanzishwa kwake. Ikiwa na miaka Zaidi ya 85 imekuwa na mafanikio yafuatayo;

1.Washindi wa Ligi Kuu ya Tanzania mara 27– 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000, 2005, 2006, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2016–17.

2.Washindi wa Kombe la Tanzania mara 4 – 1975, 1994, 1999, 2015–16

3.CECAFA Club Cup/Kagame Interclub Cup mara 5 – 1975, 1993, 1999, 2011, 2012.

4.Kombe la Mabingwa la CAF – Imeshiriki mara 11
1997 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
1998 – Hatua ya Makundi (Group stage)
2001 – Hatua ya Pili (Second Round)
2006 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2007 – Hatua ya Pili (Second Round)
2009 – Hatua ya Kwanza (First Round)
2010 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2012 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2014 – Hatua ya Kwanza (First Round)
2016 – Hatua ya Pili (Second Round)
2017 –

5.Kombe la Klabu Bingwa Africa – Imeshiriki mara 11
1969 – Robo Finali (Quarter-finals)
1970 – Robo Finali (Quarter-finals)
1971 – Ilijitoa Hatua ya Pili (withdrew in Second Round)
1972 – Hauta ya Kwanza (First Round)
1973 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1975 – Hatua ya Pili (Second Round)
1982 – Hatua ya Pili (Second Round)
1984 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1988 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1992 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1996 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)

6.Kombe la Shirikisho la CAF: Imeshiriki mara 4
2007 – Hatua ya Kati (Intermediate Round)
2008 – Hatua ya Kwanza (First Round)
2011 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2016 – Hatua ya Makundi (Group stage)
2018 – Hatua ya Makundi (Group stage)

7.Kombe la CAF: Imeshiriki mara 2
1994 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1999 – Hatua ya Kwanza (First Round)

8.CAF Cup Winners’ Cup: Imeshiriki mara 2
1995 – Hatua ya Robo Finalia (Quarter-finals)
2000 – Hatua ya Kwanza (First Round)

YANGA SC KATIKA HARAKATI ZA UKOMBOZI WA TANGANYIKA NA MUUNGANO WA TANZANIA, CHINI YA MZEE NYERERE NA KARUME.

YANGA ni klabu iliyoshiriki kwa nguvu katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika ambao baadae ulipatikana mwaka 1961 na kujiondoa kwenye mikono ya Waingereza waliokuwa watawala.

Sehemu moja ya kuonyesha kuwa kweli Yanga ilishiriki ni nembo yake ambayo hadi leo imekuwa na alama ya Bara la Afrika ikiwa ni sehemu ya kusisitiza kuwa Waafrika wanapaswa kujitegemea bila ya kuongozwa na watu kutoka nje ya bara hilo.

Historia ya Yanga SC 1935

Wakati wa utawala wa kikoloni, hakukuwa na nafasi ya kutosha kwa Waafrika kusimama na kujieleza kuhusiana na walichotaka kwa uwazi, badala yake mambo mengi yalilazimika kufanyika kwa siri kuhofia adhabu kutoka kwa wakoloni.

Jina la Young African ilikuwa ni sehemu ya dhana, kwamba linawabeba Waafrika vijana, hivyo ikawa rahisi kuihusisha klabu na wazalendo waliokuwa wakitaka kwa dhati uhuru wa nchi yao ambao ulikuwa lazima upiganiwe.

Kuanzia mwaka 1951, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikaribishwa na wazee waliokuwa Yanga na walikuwa tayari kushirikiana naye. Baadhi yao ni akina Dunstan Omar, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faiz Mafongo, Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Juma Sultan ‘Mabosti’, Said Chaurembo, Sheikh Jumbe Tambaza, Bibi Titi Mohammed, Tatu Binti Mzee na wengine wengi.

Wakati huo Nyerere alikuwa mwalimu katika Sekondari ya St Francis (sasa Pugu), mikutano ilianza kufanyika kwenye makao makuu ya Yanga ikiwa inahamasisha Watanganyika kuzungumzia unyonge wao ndani ya nchi yao na baada ya hapo kuanza kudai uhuru.

Mkutano hiyo haikuwafurahisha wakoloni hata kidogo, mara nyingi walituma mashushushu na kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea ndani. Lakini Nyerere na wenzake wa Yanga waliamua kubuni mbinu tofauti kuwakwepa.

Kwa kuwa hakukuwa na ujanja wa kuhama katika eneo hilo na kufanya mikutano kwingine, mbinu mbadala moja wapo ilikuwa ni kukifanya kikundi cha taarabu cha Jipisheni kuendelea kutumbuiza kila walipoanza vikao.

Kikundi hicho ambacho baadae kilipewa jina la Egyptian Musical Club, kiliendelea kutumbuiza huku watu wakishangilia kwa nguvu.

Ingawa kelele zilikuwa juu, lakini Nyerere na wanachama wengine wa Yanga ambao pia walikuwa wanachama wa Tanu waliendelea na mikutano yao kuhakikisha wanafikia malengo.

Mwasisi wa kikundi hicho cha taarabu, Maalim Bom Hambaroni, yeye alijitolea ikiwa ni sehemu ya mchango wake na wanamuziki wa kikundi hicho wakakubaliana na hilo kila mmoja akiwa amepania kuona siku moja wanakuwa huru.

Baadhi ya wanamuziki wa kikundi hicho na wanachama wa Yanga walipokezana kuimba huku wengine wakipika chakula ambacho Nyerere, viongozi wa Yanga na wanachama wa Tanu walikula na baadae kuendelea na vikao vyao hivyo vya ukombozi wa Tanganyika.

Mara kadhaa, katika baadhi ya mechi, klabu ya Yanga ilitoa kiasi cha fedha na kuhakikisha kinaisaidia Tanu katika mambo yake kadhaa ya kichama kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa uhuru.

Kutokana na ushirikiano wa juu aliokuwa akiupata kutoka Tanu na Yanga, Nyerere aliamua kuacha kazi yake ya kufundisha ili apate nafasi ya kutosha kupambana kusaidia kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika.

Alianza kuzungumza kila sehemu Tanganyika, dereva akiwa ni Said Tanu, ambaye alikuwa shabiki wa ‘kulia’ wa Yanga na aliwahi kueleza kwamba nje ya siasa, mwalimu alizungumza sana kuhusu mpira na Yanga ndiyo iliyokuwa ikiukosha moyo wake.

Baadaye kwa ushirikiano wa Tanu, wananchi wengi, Nyerere alifanikiwa kuipatia Uhuru wa Tanganyika, rasmi December 09 mwaka 1961.

Uhuru wa Zanzibar:

Uhuru wa Zanzibar pia Yanga ilishiriki kwa kuwa mwanamapinduzi namba moja, Abeid Amani Karume alikuwa anapenda sana mpira na ndiye mwanzilishi wa klabu ya African Sports ya Zanzibar.

Wakati fulani hata kabla ya uhuru wa Tanganyika, viongozi wa Yanga walialikwa Zanzibar na Karume. Wakiwa kule Yanga na African Sports, wakafanya mkutano wa kutaka kudumishwa undugu kwa watu wa Bara na wale wa visiwani.

Mikutano ilikuwa miwili, mmoja ulifanyika Zanzibar na mwingine ukafanyika Dar es Salaam, lengo lilikuwa ni hilo kusaidia kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika pia Zanzibar.

Mfano timu hizo ziliandaa mapambano mawili, moja likachezwa visiwani na fedha zikaichangia ASP kuendelea kupambana dhidi ya wakoloni, halikadhalika mechi nyingine ikapigwa Bara na fedha zikaisaidia Tanu kwa lengo lilelile.

Katika mechi iliyochezwa Kajengwa Makunduchi, Zanzibar na ile ya Ghymkhana (sasa Karume), watazamaji walikuwa wakiingia wanalipa kwa kuweka fedha kwenye vibubu moja kwa moja ili kudhibiti mapato.

Ndiyo maana hata baada ya Zanzibar kupata uhuru, Karume alikuwa akizialika ikulu klabu za Yanga, Simba, African Sports ya Tanga na ile ya Zanzibar kwenda kusherekea Sikukuu mbalimbali kama pasaka au Idd.

Kwa hayo hii ni sehemu ya kuonyesha Yanga ilishiriki kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa uhuru wa Tangayika, Zanzibar au Tanzania kwa ujumla na ndiyo maana ilipewa jina la timu ya wananchi.

Muungano:

Yanga inaelezwa kuwa sehemu iliyochangia kwa kiasi fulani kupatikana kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulizaa Tanzania. Maana ndiyo zilichangia Nyerere na Karume kuwa karibu na suala la kuungana likaanza.

Kwa kuwa Nyerere na Karume, wote waliamini jambo moja kuwa kuungana ni kuongeza nguvu, hivyo waliweza kuzungumza kwa urahisi zaidi kwa kuwa waliona walikuwa na sera zinazofanana.

Hivyo suala la muungano halikuwa na ugumu na ikawa pia rahisi kwa Tanu na ASP kuungana na kutengeneza Chama cha Mapinduzi (CCM).

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *