RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi

Filed in Makala, Michezo by on 18/02/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi

IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kipimo cha saratani ya shingo ya kizazi, Dalili za kansa ya kizazi kwa mwanamke, Dalili za saratani ya shingo ya kizazi, Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na nini, Dalili za kizazi kuharibika.

IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi

IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kipimo cha saratani ya shingo ya kizazi, Dalili za kansa ya kizazi kwa mwanamke, Dalili za saratani ya shingo ya kizazi, Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na nini, Dalili za kizazi kuharibika.

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI  NI NINI?

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi.

Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.

Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea.

Ripoti ya 2012 ya shirika la afya duniani ‘WHO’ ilisema kuwa kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi Barani Afrika, 50,000 walifariki Dunia.

NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI?

Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya ‘Human Papillomavirus’ au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma.

Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana.

BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA HATARI ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Kushiriki tendo la ndoa Katika Umri mdogo au chini ya Miaka 18.
  • Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti.
  • Utumiaji wa Sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini (Impairs Immune System).
  • Watu wenye kinga hafifu ya mwili au Magojwa kama Ukimwi.
  • Uzazi wa Mara kwa Mara
IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kipimo cha saratani ya shingo ya kizazi, Dalili za kansa ya kizazi kwa mwanamke, Dalili za saratani ya shingo ya kizazi, Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na nini, Dalili za kizazi kuharibika.

IJUE Saratani ya Shingo ya Kizazi

BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Kutokwa na Majimaji au Uchafu wenye harufu kali Ukeni.
  • Kutokwa na damu Ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa.
  • Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( Pelvic Area).
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa Kujamiiana.
  • Kupungua kwa uzito wa mwili bila Kukusudia.
  • Mkojo wenye matone ya damu

JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA?

Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.

PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST); Pap-Smear ni kipimo ambacho hutumika kuchunguza mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.

UMRI WA KUPATA PAP TEST

Test hii hushauriwa kwa mwanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65 na chini ya umri wa miaka 21 endapo ameingia katika tendo la ndoa kwa kipindi kisichopungua miaka 3.

KUPUNGUZA HATARI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Pap Tests.

Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3, hii itategemea ushauri wa daktari, umri, hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.

  • Pata HPV Vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa Daktari) .
  • Kuwa na mpenzi mmoja.
  • Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.
  • Tumia kinga (Condoms). hii husaidia kupunguza maambukizi ya magojwa ya zinaa

Madhara ya saratani ya shingo ya kizazi, Kansa ya Kizazi husababishwa na nini, Saratani ya shingo ya kizazi in english, Kansa ya kizazi kwa mwanaume, Picha ya shingo ya kizazi, Uvimbe kwenye shingo ya kizazi, Dalili za kizazi kuuma.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , , ,

Comments are closed.