INEC Walioitwa kwenye Usaili Iramba District Council
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Iramba Magharibi anapenda kuwatangazia wananchi wote walioomba kazi za Mwandishi Msaidizi na Mwendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki (BVR) katika Tangazo la nafasi za muda za watendaji wa vituo vya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura la tarehe 15 Aprili, 2024 kwamba waombaji wote waliokidhi vigezo kufika kwenye usaili kuanzia tarehe 04.09.2024 hadi tarehe 07.09.2024.
MAELEZO YA JUMLA KWA WASAILIWA WOTE
Usaili wa Mahojiano utafanyika kuanzia tarehe 04.09.2024 hadi tarehe 07.09.2024 kuanzia saa 2:00 Asubuhi kwa mchanganuo wa makundi yafuatayo;
KUNDI LA KWANZA – TARAFA YA SHELUI
Wasailiwa kutoka Tarafa ya Shelui inayojumuisha Kata za Shelui, Mtoa, Ntwike na Mgongo watafanya usaili tarehe 04.09.2024 katika Shule ya Msingi Tyuta.
KUNDI LA PILI TARAFA YA NDAGO
Wasailiwa kutoka Tarafa ya Ndago inayojumuisha Kata za Ndago, Ndulungu, Mtekente, Urughu, Mbelekese na Kaselya watafanya usaili tarehe 05.09.2024 katika Shule ya Sekondari Ndago.
KUNDI LA TATU-TARAFA YA KINAMPANDA
Wasailiwa kutoka Tarafa ya Kinampanda inayojumuisha Kata za Ulemo, Kyengege, Kinampanda, Maluga na Mukulu watafanya usaili tarehe 06.09.2024 katika Shule ya Sekondari Kizaga.
KUNDI LA NNE – TARAFA YA KISIRIRI
Wasailiwa kutoka Tarafa ya Kisiriri inayojumuisha Kata za Kiomboi, Old Kiomboi, Kisiriri, Tulya na Kidaru watafanya usaili tarehe 07.09.2024 katika shule ya Sekondari Kisiriri
Pamoja na Tangazo hili, orodha ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini;
Aidha kila mwombaji afike na vyeti vyake halisi (original certificates)
DONWLOAD PDF KUITWA KWENYE USAILI INEC – IRAMBA DC