INEC Walioitwa kwenye Usaili Singida District Council
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Singida Kaskazini anapenda kuwajulisha kuwa wafuatao wameitwa kwenye usaili wa nafasi za Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Biometrick(BVR KIT OPERATORS) katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaofanyika kwa siku mbili (2) katika vituo vinne(4) viliyopendekezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuanzia Tarehe 04.09.2024 hadi 05.09.2024 kama inavyoeleza hapa chini.
KUNDI A
Kata za Mgori, Mughunga, Ngimu, Itaja na Mughamo. Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 04.09.2024 saa 2:00 Asubuhi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein uliopo kata ya Mgori Tarafa ya Mgori kwaajili ya usaili.
KUNDI B
Kata za Kinyeto, Kinyagigi, Merya, Msange na Maghojoa. Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 04.09.2024 saa 6:00 Mchana katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Maghojoa uliopo kata ya Maghojoa Tarafa ya llongero kwaajili ya usaili.
KUNDI C
Kata za Mwasauya, Ikhanoda, Mrama, Ntonge na llongero. Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 05.09.2024 saa 2:00 Asubuhi katika ukumbi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Singida (Mwahango) kwaajili ya usaili.
KUNDI D
Kata za Mudida, Makuro, Mtinko, Msisi, Kijota na Ughandi. Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 05.09.2024 saa 6:00 Mchana katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mtinko uliopo kata ya Mtinko Tarafa ya Mtinko kwaajili ya usaili.
Pamoja na tangazo hili orodha ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili yameambatanishwa kwenye PDF hapa chini;
Aidha kila mwombaji afike na vyeti vyake halisi (orginal).
DONWLOAD PDF KUITWA KWENYE USAILI INEC SINGIDA DC