KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

INLAND Radio yaanzisha Timu yake

Filed in Usajili, Michezo by on 28/04/2024 0 Comments

INLAND Radio yaanzisha Timu yake

INLAND RADIO YAANZISHA TIMU YA MPIRA WA MIGUU "INLAND FOOTBALL CLUB"INLAND Radio yaanzisha Timu yake, Kutokana na umuhimu wa kujali vipaji vya wanamichezo wachanga, Kituo Cha Radio ya Inland kupitia kipindi chake cha Michezo kiitwacho Bunge la Michezo ambacho kinaruka kila Jumatatu hadi Jumapili kimeanzisha timu yake ambayo kimeipa jina la Inland Football Club.

Zoezi la usaili wa wachezaji watakaounda timu hiyo limefanyika leo 27 April 2024 katika Uwanja wa Kanisa la Baptist liliko Kona ya Bwiru Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Aidha Jumla ya Wachezaji Kumi na tano (15) wamechaguliwa kutengeneza kikosi hicho ambacho kitaanza kucheza mechi mbalimbali za Kirafiki ili kuleta Ushirikiano wa Radio hiyo na Jamii kwa ujumla ambayo ndio wateja wa vipindi vya radio hiyo.

Vigezo vya usaili huo ulikuwa kuchukua Fomu kisha mhusika kuijaza na kuirudisha.

Pia suala la umri lilizingatiwa kwa wachezaji hao maana hata Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetoa maelekezo kuandaa timu kwa umri usiozidi miaka 20.

Baada ya usaili kukamilika sasa linafuata zoezi la mazoezi ya kuandaa timu.

Mazoezi hayo yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Kitangili iliyoko Bwiru Mwanza.

INLAND Radio yaanzisha Timu yake

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *