ISHU ya Lameck Lawi na Simba Yafikia hapa
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
ISHU ya Lameck Lawi na Simba Yafikia hapa
ISHU ya Lameck Lawi na Simba Yafikia hapa,Wakati Simba ikianza safari ya kuelekea Misri kwaajili ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2024/2025, beki Lameck Lawi yeye yupo Jijini Dar es Salaam na timu yake ya Coastal Union.
Lameck Lawi yupo Jijini humo akijifua na Wachezaji wengine wa Coastal Union tayari kwa Michuano ya Kagame huku akisema yeye ni Mchezaji halali wa Coastal Union.
Lawi ambaye alikuwa wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba kuelekea msimu ujao wa 2024/2025 inaelezwa dili lake hilo limekufa kutokana na ukiukwaji wa utaratibu wakati wa usajili wake baada ya pande mbili kushindwa kuelewana mwishoni..
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Lwi alisaini mkataba wa awali wa miaka mitatu ambao uliitaka Simba kuingiza fedha kwenye akaunti ya Coastal Union Mei 31-2024, lakini timu hiyo haikufanya hivyo ndani ya muda husika.
Baada ya kubaini Simba wameenda kinyume na makubaliano klabu ya Coastal Union ilimtaka mchezaji arudishe kiasi cha fedha alichoingiziwa na wao wakarudisha kiasi kilichoingizwa kwenye akaunti ya timu ili waendelee na mambo mengine ikiwa ni pamoja na kusitisha biashara hiyo kufanyika.
Kuhusu ishu ya Lawi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, alisema kuwa, ishu ya Lawi bado ina utata hivyo suala lake litatolewa ufafanuzi hapo baadae.