JEAN Charles Ahoua Kumrithi Clatous Chama Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JEAN Charles Ahoua Kumrithi Clatous Chama Simba
JEAN Charles Ahoua Kumrithi Clatous Chama Simba, Klabu ya Simba imetajwa kuwa Katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa wa Kiungo, Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjame ya Kwao Ivory Coast.
Ahoua ndiye Mchezaji bora (MVP) kwenye Ligi Kuu nchini Ivory Coast, akichezea Klabu ya Stella Club d’Adjame ya nchini humo, ambapo amefunga mabao 12 na asisti tisa, hivyo kuhusika katika jumla ya mabao 21 msimu wa 2023/2024.
Ahoua ambaye anatajwa kuwa mrithi sahihi wa Chama, anacheza nafasi za kiungo mshambuliaji, namba 10.
Mchezaji huyo mwenye umri miaka 22, alizaliwa Februari 10, 2002 nchini Ivory Coast, na alianza soka la ushindani, mwaka 2020 alipocheza kwenye Klabu ya LYS Sassandra na mwaka huo huo, akahamia Sewe FC, ambayo alikipiga nayo hadi 2022, alipojiunga na Stella Club d’Adjame kabla ya kuwavutia Simba SC.