JEAN Othos Baleke ni Mwananchi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JEAN Othos Baleke ni Mwananchi
JEAN Othos Baleke ni Mwananchi, Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo, Jean Othos Baleke Kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Baada ya Kukamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Clatous Chama kutoka Simba na Mshambuliaji Prince Dube aliyevunja Mkataba wake na Azam FC, Klabu hiyo imekamilisha usajili wa, Jean Othos Baleke aliyewahi kuichezea Simba SC.
Baleke mwenye umri wa miaka 23 aliachwa na Simba baada ya mkataba wake mkopo kutoka TP Mazembe kumalizika na kutimkia Al Ittihad ya Libya ambayo imetwaa taji la Ligi Kuu msimu wa 2023/2024.
Young Africans imefikia maamuzi ya kumsajili Bakeke baada ya kuachana na dili la Jonathan Sowah ambapo wanaamini Baleke anaifahamu vizuri Ligi kwani uwezo wake umeonekana akiwa Simba kabla ya kutimkia Libya.