JEZI Mpya za Azam FC 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JEZI Mpya za Azam FC 2024/2025
JEZI Mpya za Azam FC 2024/2025, Klabu ya Azam Football Club imetambulisha jezi zake za msimu mpya kwenye boti ya Kilimanjaro Eight ‘The Falcon Sea’ wakati wa safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Ni jezi aina tatu zenye mvuto, uimara na ubora wa hali ya juu, ikiwa ya kwanza ni ya nyumbani, ambayo ni ya rangi nyeupe na dhahabu, ya pili ni ya ugenini yenye rangi ya blue na dhahabu, na ya tatu ni nyeusi na dhahabu maarufu Third Kit.
Azam walizindua rasmi jezi hizo kwenye jengo la Michenzani Mall, Unguja, visiwani Zanzibar ambako mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi, Tabia Maulid Mwita.