RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


JINSI ya kubadili taarifa zako Ajira Portal

Filed in Ajira by on 12/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

JINSI ya kubadili taarifa zako Ajira Portal

JINSI ya kubadili taarifa zako Ajira Portal,Jinsi ya kubadili taarifa ajira Ajira Portal Jinsi ya kuedit document kwenye mfumo wa Ajira Portal, Jinsi ya kurekebisha nakala zako kwenye mfumo wa Ajira Portal UTUMISHI.

JINSI ya kubadili taarifa zako Ajira Portal

JINSI ya kubadili taarifa zako Ajira Portal,Jinsi ya kubadili taarifa ajira Ajira Portal Jinsi ya kuedit document kwenye mfumo wa Ajira Portal, Jinsi ya kurekebisha nakala zako kwenye mfumo wa Ajira Portal UTUMISHI.

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 iliyorejewa 2019, ambayo inaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Jukumu la msingi la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kuwezesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbalimbali za Umma.

Hivi karibuni zimetangazwa nafasi za kazi mbalimbali na watanzania wenye sifa wanatakiwa kuomba nafasi hizo kupitia mfumo wa Ajira Portal.

Katika mfumo huo muombaji anatakiwa kupakia nakala za vyeti vyake ambazo zimehakikiwa na kugongwa mhuri na Mwanasheria au Wakili kuonesha kuwa ni nakala kutoka katika vyeti halisi.

Pia Muomba kazi anatakiwa kupakia vyeti vyake kwenye mfumo kulingana na kiwango chake cha Elimu ili kumuwezesha kuomba pindi nafasi zinapo tangazwa.

Ikitokea umeudanganya mfumo au umeweka cheti cha taaluma kisicho cha kwako, au unataka kuomba nafasi ya juu au ya chini kulinganisha na cheti cha taaluma ulichonacho, hutoweza kuomba nafasi uliyoomba kwani mfumo unatambua cheti chako cha elimu ambacho umeweka kwenye mfumo.

Ikitokea umekosea kupakia cheti chako, Mfumo hauto kuruhusu kufuta cheti chako bali utalazimika kwenda sehemu uliyokosea na kuhariri (edit) cheti chako kisha kupakia tena (upload) kilicho sahihi.

Hata hivyo; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetambua changamoto wanazokutana nazo waombaji kazi na imeweka simu ya huduma kwa mteja namba 0262160350 inayopatikana kuanzia saa 2.00 Asubuhi mpaka saa 12.00 Jioni kwa siku za kazi na Maafisa wapo tayari kwaajili ya kutoa huduma pia unaweza kutuma barua kupitia ict@ajira.go.tz.

Pia kwa Msaada zaidi unaweza kufika katika Ofisi zetu zilizopo Dodoma katika majengo ya Dr. Asha Rose Migiro, Dar es Salaam – Magogoni, na Zanzibar – Mazizini (Jengo la sheria, Ghorofa ya tatu) kwa ajili ya msaada zaidi.

Aidha, tunawasihi waomba kazi kujaza taarifa na kupakia nakala za vyeti vyao kwenye mfumo wa Ajira portal wao wenyewe na si kufanyiwa na mtu mwingine ili kuepuka makosa yanayoweza kuepukika, na pia mnatakiwa kuzingatia taratibu na masharti yaliyoekwa kwani watanzania wengi wameweza kuomba kazi na kufanikiwa.

Epuka Matapeli, soma maelekezo kabla ya kupakia vyeti vyako na kuomba nafasi ya kazi uliyo kusudia.

Lynn Chawala
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.