RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


JINSI ya Kujisajili SimBanking App

Filed in Makala by on 29/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

JINSI ya Kujisajili SimBanking App

JINSI ya Kujisajili SimBanking App

JINSI ya Kujisajili SimBanking App

JINSI ya Kujisajili SimBanking App, Tuko nawe masaa 24, siku 7 za wiki uendako na SimBanking inayokuwezesha kufanya miamala yako kwa kutumia simu ya kiganjani muda wowote, mahali popote.

SIFA za Kuwa na SimBanking

  • Kuhamisha pesa kwenda akaunti yoyote ndani ya mtandao wa benki ya CRDB.
  • Kutuma pesa kwenda mitandao ya simu
  • Kutuma pesa kenda benki nyingine
  • Kulipia bili na malipo ya serikali (GePG) (Brela, TPA, TRA, Luku, Dawasco/Moruwasa, Startimes, SUA n.k.)
  • Kulipia bima
  • Mikopo ya haraka bile kufika tawini
  • Kununua muda wako maongezi ama kuwanunulia wengine.
  • Kutuma pesa kwa mtu asiyekuwa na akaunti benki au kadi ya ATM.
  • Kuuliza salio bure.
  • Taarifa fupi na taarifa za akaunti yako mpaka mwaka mmoja
  • Kupata taarifa za matumizi ya TemboCards/Visa/ MasterCard.
  • Kufunga na kufungua TemboCard yako
  • Kujifungulia akaunti ya benki ya CRDB
  • Una uwezo wa kujisajili.
  • Una uwezo wa kubadili namba ya siri.
  • Una uwezo wa kubadili lugha, Kiswahili au Kiingereza.

Usalama Unapokuwa na SimBanking App

Huduma ya SimBanking ni salama na uhakika. Miamala yote utakayoifanya itahitaji namba yako ya siri.

Hata kama mtu mwingine akitumia simu yako hawezi kufanya miamala bila kutumia namba yako ya siri(PIN).

JINSI ya Kujisajili SimBanking AppFaida unazozipata ukiwa na SimBanking App

  • Una uwezo wa kutumia akaunti yako wakati wowote, popote ulipo. Kuhamisha pesa kwa wapendwa wako bila kuhangaika.
  • Kulipia bili zako kiurahisi zaidi.
  • Lipa washirika wako wa biashara na wagavi wako bila wasiwasi.
  • Panua wigo wa matumizi ya simu yako.
  • Fanya miamala yako muda wote.
  • Uwezo wa kujifungulia akaunti ya CRDB popote ulipo
  • Kupata mikopo ya haraka bila kujaza fomu wala kufika tawini

Jiunge na huduma ya SimBanking App kwa kufuata maelekezo yafuatayo;

  • Pakua App ya SimBanking
  • Ingiza PIN ya SimBanking
  • Ingiza namba yako ya akaunti
  • Ingiza PIN ya mara moja
  • Kupata OTP, piga *150*03#
  • Ingiza SimBanking PIN
  • Chagua namba 7 “Huduma za ziada”
  • Chagua namba 4 “Sajili SimBanking App”
  • Utapokea sms yenye OTP
  • Itumie PIN hiyo kujisajili kupitia App ya SimBanking, inatumika ndani ya dakika 5 tu.

Pakua App ya SimBanking hapa https://bit.ly/simbanking kupitia PlayStore ukiwa na simu ya Android au App Store ukiwa na simu ya iOS au piga *150*03# kupata menu ya SimBanking.

Vigezo na Masharti

  • Unapaswa kuwa na akaunti ya Benki ya CRDB au fungua akaunti mpya. Unaweza kuwa na akaunti ya akiba au akaunti ya Hundi.
  • Wateja wote wa Benki ya CRDB wanaweza kutumia huduma hii bila kujali wanatumia mtandao gani wa simu au aina ya simu.
  • Kujisajili ni haraka na rahisi sana, tumia njia maoja wapo kati ya hizi;
  • Piga *150*03# kisha fuata maelekezo ya namna ya kujiunga
  • Tumia TemboCard yako kujisali SimBanking kupitia ATM zetu zilizoenea nchi nzima.
  • Kama hauna TemboCard tembelea tawi la karibu yake tutakuunganisha na SimBanking.

Maswali

Je! ni mipaka gani ya manunuzi kwa shughuli za simbanking katika tzs?

  • Uhamisho wa fedha kwenda mitandao ya Simu – Milion mbili (2) kwa kila muamala, kwenda akaunti nyingine ya benki ya CRDB – Milioni nane (8), kwenda akaunti yako nyingine ya benki ya CRDB – Milioni kumi (10) kwa siku, Muda wa maongezi – Laki mbili (2) kwa muamala, Kutoa pesa kwenye ATM (Cardless) – Milioni 1, Kutoa pesa tawini bila kujaza karatasi (Paperless) – Milioni ishirini (20)
JINSI ya Kujisajili SimBanking App

JINSI ya Kujisajili SimBanking App

Ninawezaje kubadilisha namba yangu ya simu iliyosajiliwa ya simbanking?

  • Kupitia Usajili kwenye ATM. Sehemu ya 1 – kwenye ATM Tembelea ATM ya CRDB Ingiza kadi ya ATM na uweke PIN Chagua huduma zingine Chagua usajili wa SimBanking Chagua Mabadiliko ya Nambari ya Simu Chagua akaunti Ingiza nambari ya simu iliyosajiliwa hapo awali Ingiza nambari mpya ya simu Thibitisha maelezo Utapokea SMS na PIN ya awali Sehemu ya 2 – Kwenye namba mpya ya simu 1. Piga * 150 * 03 # 2. Ingiza nambari ya akaunti 3. Ingiza PIN ya awali – uliyo pokea kwenye SMS 4. Thibitisha PIN Kupitia matawi ya CRDB ya Karibu bila hitaji la Kadi ya ATM.

Je naweza kutuma pesa kwenda benki nyingine (tss) kwa kutumia simbanking ussd (*150*03#)?

  • Ndiyo. Piga * 150 * 03 #, kisha weka PIN Chagua Chaguo 2. Tuma pesa Chagua Chaguo 3. Benki zingine 4. Chagua akaunti ya kutumika 5. Andika herufi tatu za kwanza za benki nyingine 6. Chagua Benki 7. Ingiza akaunti ya walengwa, Kisha Jina la mlengwa, kisha Kiasi Thibitisha.

Je! najisajili vipi na simbanking app?

  • Unahitaji kusajiliwa kwenye SimBnking USSD (* 150 * 03 #) kisha, Pakua SimBanking App kupitia Google Play store au App Store. Kisha weka namba ya akaunti iliyounganishwa na simbanking USSD (*150*03#), namba ya simu iliyounganishwa na SimBanking USSD (* 150 * 03 #), Weka namba ya siri ya simbanking( PIN) kisha weka pini ya maramoja(OTP). Ili kupata OTP piga * 150 * 03 #, chagua 7, huduma kisha, chagua 4, usajili wa App App. Ndani ya masaa 24 utapata OTP ilikukamilisha usajili kwa kuweka namba ya simu ya SimBanking, namba ya siri ya SimBanking kisha OTP iliyotumwa kwenye ujumbe mfupi(sms).

Ninawezaje kuzuia / kufungia kadi yangu ya ATM

  • Ingia kwenye SimBanking App, Chagua kadi ya kufunga, chagua zuia kadi kisha funga kadi

Je! ni kiwango cha chini na cha juu kabisa kuhamishia (mnos, akaunti za crdb na benki zingine)?

  • Uhamisho wa fedha kwenda mitandao ya Simu – Milion mbili (2) kwa kila muamala, kenda akaunti nyingine ya benki ya CRDB – Milioni nane (8), kwenda akaunti yako nyingine ya benki ya CRDB – Milioni kumi (10) kwa siku, Muda wa maongezi – Laki mbili (2) kwa muamala, Kutoa pesa kwenye ATM (Cardless) – Milioni 1, Kutoa pesa tawini bila kujaza karatasi (Paperless) – Milioni ishirini (20)

Je! ninaunganishaje akaunti zangu zingine?

  • Ingia kwa SimBanking App Bonyeza mipangilio Chagua unganisha akaunti zangu zingine Tiki akaunti hizo na ubonyeze thibitisha

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.